The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

5 2 /

UFALME WA MUNGU

7. Mungu alifanya upya agano la Abramu kupitia kabila gani katika Israeli? Katika kabila hilo, ni familia gani ambayo kupitia kwayo tunasoma kwamba Masihi aliahidiwa kuja? 8. Kulingana na Kutoka 19, Mungu alikuwa na kusudi gani kwa watu wake Israeli? Israeli walifanyaje katika jukumu lao la kuwa nuru kwa mataifa kwa niaba ya Mungu Mwenyezi? 9. Yesu wa Nazareti ana uhusiano gani na mzao wa Abramu? Na, je, Yesu wa Nazareti ana uhusiano gani na Uzao wa mwanamke aliyetajwa katika proto-evangelium ?

Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu Sehemu ya 2

2

Mch. Dkt. Don. L. Davis

Mungu amekuwa akifanya kazi tangu mwanzo ili kukomesha kutotii na uasi wote ambavyo ni matokeo ya Anguko, kupitia kufunuliwa kwa ahadi yake ya agano kwa Ibrahimu ya kuleta Mzao. Ahadi hii inaweza kufuatiliwa kupitia watu wa Mungu wa agano, kupitia Yuda, Daudi. Ijapokuwa watu wa Mungu walishindwa kiadili na kuabudu sanamu, kupitia kwao alitokea Mpakwa Mafuta, Yesu wa Nazareti, anayewakilisha kutimizwa kwa ujio wa Ufalme. Kwa uwezo na mamlaka ya mwisho, utawala wa Mungu umedhihirishwa kupitia kuvaa mwili kwa Yesu, kifo, ufufuo, na kupaa kwake. Lengo letu katika sehemu hii ya pili ya somo hili la Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Katika nafsi na kazi za Yesu wa Nazareti, Utawala wa ufalme wa Mungu umezinduliwa kwa utukufu (katika maana ya mwisho), na kutimizwa ulimwenguni. • Yesu alitoa ushahidi na uhai kwa utawala wa Mungu kama Christus Victum kwa njia ya mateso, kifo, na kuzikwa kwake. • Yesu alitoa uthibitisho usiopingika wa kuzinduliwa na kutimizwa kwa Ufalme kama Christus Victor kupitia ufufuo wake wenye utukufu na kupaa kwake.

Muhtasari wa Sehemu ya 2

ukurasa 323  9

Made with FlippingBook Learn more on our blog