The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
6 2 /
UFALME WA MUNGU
9. Kama ishara ya mamlaka na Ukuu wa Yesu, kupaa kunachangiaje uelewa wetu kwamba katika Yesu, Ufalme umezinduliwa?
MUUNGANIKO
Somo hili linaangazia njia muhimu ambazo Agano la Kale na Agano Jipya zinashuhudia kwamba Ufalme wa Mungu umezinduliwa, kupitia ahadi ya agano la Mungu kwa Ibrahimu na Mababa, kupitia kabila la Yuda na ukoo wa Daudi, na hatimaye katika Yesu Kristo, ambaye kama Christus Victum (yaani kupitia kifo chake msalabani) na Christus Victor (yaani kupitia ufufuo wake na kupaa kwake) ameuingiza Ufalme wa Mungu katika enzi hii ya sasa. ³ Mungu tangu mwanzo alidhamiria kupindua athari za Anguko kwa kuwa Shujaa dhidi ya adui zake, akimpinga nyoka huku akitoa neema kwa Uzao wa mwanamke ambao ungekuja na kuwashinda adui zake. ³ Proto-evangelium (rej. Mwa. 3:15) inawakilisha tangazo la kwanza na kuu zaidi la dhamira ya Mungu wa Utatu kumshinda adui yake, nyoka, kupitia Uzao wa mwanamke, ambaye sasa tunamjua kuwa Yesu wa Nazareti, Bwana wa wote. ³ Mungu akiwa Shujaa wa Kiungu alifanya agano na Abrahamu kubariki familia zote za dunia kupitia Mzao wake, ambaye tunamjua sasa kuwa ni Yesu wa Nazareti. ³ Mungu alifanya upya ahadi yake ya agano kutoka kwa Abrahamu, kwenda kwa Isaka na Yakobo, kwa watu wa Israeli, kwa kabila la Yuda, kwa ukoo wa Daudi, na hatimaye kupitia Yesu Kristo, ambaye ametimiza Ufalme katika maana ya mwisho kupitia maisha na kazi yake. ³ Katika Yesu wa Nazareti, ahadi za agano za Ibrahimu na ahadi za kinabii za ushuhuda wa Agano la Kale kwa habari ya Masihi zimetimizwa. Yesu ndiye utimilifu wa ahadi ya Kimasihi. ³ Katika maisha na huduma ya Yesu, mamlaka na nguvu za utawala wa Mungu zimezinduliwa na kudhihirishwa. Ijapokuwa sehemu kubwa ya utimilifu wa Ufalme huo ni ya wakati ujao, tayari Ufalme huo umedhihirishwa katika umwilisho wa Yesu duniani.
Muhtasari wa Dhana Muhimu
2
Made with FlippingBook Learn more on our blog