The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 6 1

UFALME WA MUNGU

Hitimisho

ukurasa 326  12

» Yesu wa Nazareti ndiye mkuu zaidi, Mpakwa-Mafuta wa Mungu ambaye kupitia yeye ahadi za Ibrahimu zimetimizwa. » Ndani yake, Bwana wa wote, uwepo wa Ufalme ulidhihirika, na kuonyeshwa kupitia kuvaa kwake mwili, kifo, ufufuo, na kupaa kwake.

Maswali yafuatayo yamekusudiwa kukusaidia upitie maudhui yanayohusiana na Yesu kuzindua na kutimiza Ufalme wa Mungu. Jibu maswali, ukikazia fikira kwenye “mawazo makuu” na kanuni zinazohusiana na wazo la kuzinduliwa kwa Ufalme, na pia jukumu la Yesu katika kuleta Ufalme katika uhalisia. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko! 1. Ni kwa njia zipi inaweza kusemwa kwamba Yesu wa Nazareti alijitangaza kuwa utimilifu wa ushuhuda wa Agano la Kale kwa habari ya Masihi? 2. Ni zipi baadhi ya ishara katika maisha ya Yesu zinazothibitisha kwamba ndani yake Ufalme umezinduliwa na kutimizwa kwa kiwango fulani? 3. Elezea uhusiano uliomo katika kifungu cha maneno, “Ufalme ambao upo tayari/ambao haujakamilika”. Ni katika njia zipi Ufalme unaweza kusemwa kuwa tayari upo? Ni katika njia zipi tunaweza pia kujua kwamba Ufalme bado uko katika wakati ujao? 4. Nini maana ya neno parousia , na linahusianaje na wazo zima la Ufalme ambao bado unakuja? 5. Je, Yesu analinganishwaje na Mwana-Kondoo wa Pasaka wa sherehe ya Agano la Kale? Ni katika njia zipi Yesu angeweza kusemwa kuwa ni Mwana-Kondoo wa Pasaka wa Agano Jipya? 6. Kifo cha Kristo kinadhihirisha nguvu za Ufalme wa Mungu uliopo katika njia mbili zipi leo? 7. Kulingana na Paulo, kwa nini ufufuo ni fundisho kuu la Ukristo? Tunajuaje kwamba ufufuo wa Yesu ni hakika – kuna ushahidi gani kwa hilo? 8. Ni baadhi ya mambo gani ambayo ufufuo unamaanisha kuhusu Ufalme?

Sehemu ya 2

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

2

ukurasa 327  13

Made with FlippingBook Learn more on our blog