The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
6 0 /
UFALME WA MUNGU
4. Ufufuo wake ni njia ya kuadhimishwa kwake katika ukuu na kuinuliwa kama Kichwa cha Kanisa, Efe. 1:20-23.
5. Ufufuo wake unathibitisha kwamba kuhesabiwa haki kwetu mbele za Mungu kumetimizwa kupitia yeye pekee, Rum. 4:25.
6. Na Yesu, kama Bwana wa uzima, alifufuliwa kuwa limbuko la kundi kubwa la waamini watakaoshiriki utukufu wake wa ufufuo, 1 Kor. 15:20-23.
E. Kupaa ni ishara inayoonekana ya mamlaka na ukuu wa Yesu, kuinuliwa kwake kama Shujaa wa ushindi wa Mungu, na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Mungu. Sambamba na kuanzishwa kwa Ufalme wa Mungu kupitia Yesu wa Nazareti, Yesu amepaa mbinguni. Kwa nini?
2
1. Kama ishara inayoonekana ya mamlaka na ukuu wake, aliyeabudiwa juu na malaika watakatifu wa Mungu, Ebr. 1:3-4
2. Kama Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Mungu na Bwana wa mavuno, Mt. 28:18-20
3. Kama Kichwa cha Kanisa, Efe. 1:20-23
4. Kama ishara ya ukuu wake na ubwana kamili juu ya yote, Flp. 2:9-11
Made with FlippingBook Learn more on our blog