The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 6 9

UFALME WA MUNGU

Uvamizi wa Utawala wa Mungu

SOMO LA 3

ukurasa 329  1

Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kushiriki katika mijadala, na kutendea kazi yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kuonyesha kwamba Kanisa la Yesu Kristo, kama mwili na wakala wake, lenyewe ndilo kituo (mahali na/au muktadha) wa wokovu wa Mungu, wa uwepo utiao nguvu wa Roho Mtakatifu, na wa madhihirisho ya kweli ya maisha na ushuhuda wa Ufalme. • Kuona kwamba Kanisa la Yesu Kristo si tu muktadha, bali wakala, mtumishi wa Mungu aliye tayari na anayepatikana ili kuendeleza makusudi ya ufalme duniani. • Kukariri kifungu kinachohusiana na uvamizi wa utawala wa Mungu. Jeuri ya Ufalme Soma Luka 14:26-33. Hakuna mtu ambaye angetarajia Yesu kuwa mtu anayehusishwa na migogoro na vurugu. Ni vigumu sana kwa mtu mpole na mnyenyekevu kiasi kile kuonekana kama mtu ambaye jina na sifa yake vingehusishwa na matukio halisi mabaya na ya kutisha namna hii. Hata hivyo, katika maisha yake yote na huduma yake Yesu alithibitisha kwamba hakuja kuleta amani bali upanga, uliosababisha hata kutengana na kutengwa kati ya wale walioitwa washiriki wa karibu wa familia (Mt. 10:34). Alifundisha kwamba uaminifu kwake na Ufalme wake ulidai maisha yote ya mwanafunzi (Mt. 13:44-), na kwamba lazima mtu ajiondoe mwenyewe kutoka kwenye kila alichokuwa nacho ili kujisalimisha kwake kikamilifu (Mk. 10:21). Kama vile G. E. Ladd alivyodokeza, “Uwepo wa Ufalme unadai mwenendo mkali, wenye jeuri. Wanadamu hawawezi kukaa tu wakingojea ujio wa Ufalme wa eskatolojia kama Waapokaliptisti walivyofundisha. Kinyume chake, Ufalme umewajia, na wanapaswa kuuteka kwa bidii, kwa jeuri, na kwa nguvu” ( The Presence of the Future . New York: Harper and Row, 1974, uk. 164). Kuwa mfuasi ni kubeba msalaba wako, kuchukia maisha yako mwenyewe, na kuacha kila kitu ulichonacho kwa ajili ya hazina mbinguni. Mtindo wa maisha wa ufalme ambao haudai mabadiliko, na hauna jeuri si ule unaohusishwa na Mwana wa Mungu, ambaye ni Shujaa wa Mungu kwa ajili ya kurejesha utawala wa Mungu duniani. Kwa hiyo, na tusimame na kupigana kama askari waliovaa silaha zote

Malengo ya Somo

3

Ibada

ukurasa 329  2

Made with FlippingBook Learn more on our blog