The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

7 0 /

UFALME WA MUNGU

kwa ajili ya vita (Efe. 6:10-18), tukielewa kikamilifu kwamba Yesu alidhihirishwa ili kuziharibu kazi za Ibilisi (1 Yoh. 3:8). Kumpenda Yesu ni kuichukia dunia na kuweka mapenzi yako juu ya mambo yaliyo juu ambako Kristo ameketi, mkono wa kuume wa Mungu (Kol. 3:1-3). Kama mfuasi wa Yesu, jizatiti kwa nia ya kufanya vita, kwa maana vita vinaendelea! Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Baba yetu uliye mbinguni, tunalisifu Jina lako. Tunalitukuza Jina lako na tunakuomba kwamba mapenzi Yako yafanyike na kwamba nuru Yako ipate kupenya ndani ya Kanisa lako. Tunakuomba uiongoze meli yetu. Tunatamani kuwa sehemu ndogo ya Kanisa lako la kweli, Kanisa lako kuu na takatifu, na kukuomba uongoze meli hii kupitia bahari hii yenye dhoruba na kupitia hatari na mipasuko yote. Amina. ~ Henri Arnold. May Thy Light Shine . Rifton, NY: Plough Publishing House, 1985. uk. 170.

Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi

3

Weka kando vitabu na madokezo yako, kusanya mawazo na tafakari zako, na ufanye jaribio la Somo la 2, Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu .

Jaribio

Fanya mazoezi pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu kwa kutamka andiko la kukumbuka ulilopewa katika kipindi kilichopita: Luka 11:15-20.

Mazoezi ya kukariri Maandiko

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki ililopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walikusudia kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za kukusanya

MIFANO YA REJEA

Kujitoa kwa Kristo au kwa Kanisa, au Vyote?

Ungejibuje kauli hii: “Hakuna anayeweza kudai kuwa na uhusiano wa karibu sana na Yesu Kristo huku akiwapuuza au kuwakataa watu wake, Kanisa.” Katika zama hizi zilizojaa wainjilisti na wahubiri wengi kwenye luninga, Ukristo wa kibinafsi, na kurukaruka kutoka kanisa hili kwenda lile, je, kauli hii inaleta maana kwako? Wengi wanaamini kwamba ingawa kila mkristo anapaswa kuwa mfuasi wa kanisa

1

ukurasa 330  3

Made with FlippingBook Learn more on our blog