The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 7 3

UFALME WA MUNGU

2) Pia, Agano Jipya linazungumza kuhusu Kanisa kama kusanyiko au kundi la waamini katika eneo lolote, au jumuiya ya makusanyiko kama haya, kama vile 1 Wakorintho 1:2, Wagalatia 1:2, au Wafilipi 1:1. Tunayaita makusanyiko haya “makanisa ya mahali.” • Theolojia ya Imani ya Nikea kuhusu Kanisa (Eklesiolojia). 1) Kanisa ni moja lililoungamanishwa kwa imani katika Yesu Kristo. 2) Kanisa ni takatifu (Kanisa limetengwa kama watu wa Mungu kwa milki yake na matumizi yake). 3) Kanisa ni katoliki (yaani la ulimwengu wote, watu kutoka kila taifa, kabila, lugha na jamaa). 4) Kanisa ni la kitume (limejengwa juu ya msingi wa ushuhuda wa manabii na mitume walioshuhudia kwa macho).

A. Kanisa ni mlinzi wa Injili na Neno la Mungu.

3

1. Wakili wa siri za Mungu, nguzo na msingi wa kweli, 1 Tim. 3:15-16.

2. Lina ufunuo wenye mamlaka kuhusu Kristo, na utendaji wa Ufalme wake, Mt. 16:18-19.

B. Kanisa ni mahali ambapo msamaha na uponyaji wa Mungu hupatikana kwa damu ya Yesu Kristo.

1. Waaminio katika Kristo wamepokea kwa imani msamaha wa Mungu, 1 Yoh 2:12.

2. Wale walioamini wamekombolewa kutoka katika milki ya Shetani na wamepokea ukombozi, msamaha wa dhambi, Kol. 1:13.

Made with FlippingBook Learn more on our blog