The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
7 8 /
UFALME WA MUNGU
b. Ufalme ni kazi: Kanisa ni chumvi (kuhifadhi) na mwanga (kuangaza na kufichua) katika maisha ya Ufalme.
2. Kanisa ulimwenguni, Mt. 5:13-16
Hitimisho
» Kanisa la Yesu Kristo ni kituo, mahali au muktadha, wa wokovu wa Mungu. » Kanisa la Yesu Kristo ni mahali pa uwepo wa Roho Mtakatifu unaotia nguvu.
» Kanisa la Yesu Kristo ndilo eneo la maisha halisi ya ufalme.
3
Maswali yaliyo hapa chini yameundwa ili kukusaidia kutambua mambo muhimu katika sehemu ya video iliyopita kuhusu Kanisa kama kituo cha Ufalme. Tafadhali jibu maswali yafuatayo kwa umakini, kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko! 1. Ni kwa maana gani Kanisa linaweza kuitwa “jumuiya ya Mungu wa Utatu?” Ni zipi maana mbili za ekklesia (walioitwa) katika Maandiko? 2. Nini maana ya tafsiri nne za Kanisa katika Kanuni ya Imani ya Nikea? Kwa nini tafsiri hizi ni muhimu ili kulielewa Kanisa? 3. Kama mahali pa uwepo wa Roho Mtakatifu unaotia nguvu, ni kwa njia gani Roho ni “malipo ya awali” ( arrabon ) ya baraka za ufalme zijazo? Je, hii inahusiana vipi na ufahamu wa Agano la Kale kuhusu Kanisa? ( rej. kauli ya Petro siku ya Pentekoste) 4. Ni kwa maana gani inaweza kusemwa kwamba Kanisa ni “mlinzi” au “wakala” wa ufunuo wa Mungu katika Kristo? 5. Kuna uhusiano gani kati ya mwili wa Kristo na msamaha wa dhambi? Je, mtu anaweza kupata msamaha wa Mungu na asiwe sehemu ya mwili wa Kristo? Kwa nini ndio au kwa nini hapana?
Sehemu ya 1
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
ukurasa 334 8
Made with FlippingBook Learn more on our blog