The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 7 9

UFALME WA MUNGU

6. Toa mifano kadhaa kutoka katika Maandiko inayounga mkono wazo kwamba “Roho Mtakatifu wa Mungu ndiye Bwana wa Kanisa, analitia nguvu, analiongoza, na kulielekeza katika ulimwengu huu.” 7. Ni kwa njia gani Ufalme wa Mungu unaonekana na kudhihirishwa katika maisha ya Kanisa? Kwa nini ni muhimu kuthibitisha ukweli kwamba Kanisa ni mahali ambapo nguvu za Ufalme (utawala mkuu wa Mungu) hupatikana? 8. Ni kwa njia gani ni sawa kusema Ufalme ni zawadi na kazi ya Kanisa?

Uvamizi wa Utawala wa Mungu Sehemu ya 2

Mch. Dkt. Don L. Davis

3

Kanisa la Yesu Kristo ni wakala, mtumishi wa Mungu aliye tayari na anayepatikana ili kuendeleza makusudi ya ufalme wake ulimwenguni. Lengo letu la sehemu hii ya pili ya Uvamizi wa Utawala wa Mungu ni kukuwezesha kuona kwamba: • Kanisa la Yesu Kristo ni wakala, mtumishi aliye tayari na anayepatikana kwa Mungu kuendeleza makusudi ya ufalme wake ulimwenguni. • Kanisa ni wakala wa Ufalme wa Mungu kwa kumwabudu Mungu kama Mfalme na Bwana. • Kanisa ni wakala wa Ufalme wa Mungu kupitia ushuhuda wake wa kitume. • Kanisa ni wakala wa Ufalme wa Mungu kwa bidii yake kwa ajili ya matendo mema. • Kanisa ni wakala wa Ufalme wa Mungu kwa kuwa chombo cha Mungu kwa ajili ya ishara na maajabu ya kinabii.

Muhtasari wa Sehemu ya 2

ukurasa 335  9

Made with FlippingBook Learn more on our blog