The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

8 2 /

UFALME WA MUNGU

B. Tumeitwa pia kulinda na kutunza ukuu na umuhimu wa ushuhuda wa kitume kwa Yesu Kristo.

1. Imani ya Kikristo – kile ambacho Mitume waliamini na kufundisha kuhusu Kristo na Ufalme wake.

2. Mungu amekabidhi siri za imani ya Kikristo kwa Kanisa – kutetea, kueleza, na kutangaza, 2 Tim. 2:15.

3. Kuitwa kutetea imani “waliokabidhiwa watakatifu mara moja tu” na Mitume, Yuda 3.

4. Uhakika wa uwepo wa walimu wa uongo na wasikilizaji wapotovu katika Kanisa, Mdo 20:28-38; 1 Tim. 4:2-4

3

5. Kanisa linasimamia kweli ya Mungu, na kuwakabidhi mashahidi waaminifu ambao wanaweza kuandaa wengine, 1 Kor. 4:2; 2 Tim. 2:2.

C. Uinjilishaji unahusiana moja kwa moja na uwekaji muktadha: kushirikisha wengine Habari Njema kunaenda pamoja na kuitetea Habari Njema ya Ufalme, Millard Erickson.

III. Kanisa ni wakala wa Ufalme wa Mungu kupitia bidii yake katika matendo mema.

A. Kanisa liliumbwa upya katika Kristo kutenda matendo mema, na kuwa na bidii kwa ajili ya matendo mema.

1. Tutafanya matendo makuu kuliko Kristo (Yohana 14:12-13).

Made with FlippingBook Learn more on our blog