The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 8 5

UFALME WA MUNGU

4. Asili ya upinzani wa kishetani – ni nini?

a. Kuwatesa viongozi wa Kanisa

b. Kuwatisha washirika wa Kanisa

c. Kupinga ujumbe wa Injili.

5. Mateso ni kawaida kwa wale wanaoishi maisha ya utauwa katika ulimwengu wa sasa katika Kristo, 2 Tim. 3:12.

6. Kama wawakilishi wa Yesu katika ulimwengu wenye jeuri na upinzani, Roho Mtakatifu atalithibitisha Neno la Ufalme kwa ishara na nguvu za Ufalme, Mk. 16:19-20.

3

C. Nguvu za Roho Mtakatifu zitaonyeshwa wakati Kanisa likiendeleza Ufalme wa Mungu hadi miisho ya dunia.

1. Kanisa ulimwenguni kama “Kanisa Pambanaji”

a. Kanisa Pambanaji lipo katikati ya nyakati mbili, katika Ufalme ambao upo tayari/ambao haujakamilika.

b. Kanisa katika vita linawakilisha maslahi ya Kristo kama askari wanavyowakilisha nchi yao ya kigeni, 2 Tim. 2:3-4.

2. Kanisa limepewa mamlaka ya kumwakilisha Yesu kwa nguvu, kwa maana Ufalme wa Mungu hauko katika neno pekee, 1 Kor. 4:20.

Made with FlippingBook Learn more on our blog