The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
8 6 /
UFALME WA MUNGU
3. Kwa sababu Ufalme ni wa wakati wa sasa (yaani upo sasa), ndivyo ulivyo uweza wa ufufuo wa Kristo kwa ajili ya kudhihirisha uhalisia wa Ufalme ulimwenguni!
Hitimisho
» Kanisa la Yesu Kristo ndilo kitovu na uwanja wa wokovu wa Mungu, kwa ajili ya uwepo wa Roho Mtakatifu mwenye kutia nguvu, na udhihirisho wa kweli wa maisha na ushuhuda wa Ufalme. » Kanisa la Yesu Kristo ni wakala wa ibada, ushuhuda, matendo na maajabu ulimwenguni, likiuendeleza Ufalme katika nguvu za Roho Mtakatifu.
Maswali haya yameundwa ili kukusaidia kufanya marudio na kujadili ukweli kuhusu Kanisa kama wakala wa maisha na uwepo wa Ufalme ulimwenguni leo. Tafadhali chukua muda mwingi uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yaliibuka kutokana na maudhui ya video. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko. 1. Nini maana ya neno “wakala”? Je, Kanisa linafanya kazi vipi kama wakala wa Ufalme wa Mungu katika kumwabudu Mwenyezi Mungu? 2. Kwa nini ibada ni muhimu sana kwa utambulisho na wajibu wa Kanisa ulimwenguni? Je, Kanisa linaweza kutimiza kazi yake ulimwenguni ikiwa litashindwa kuwa mwabudu halisi wa Mungu? Kwa nini ndio au kwa nini hapana? 3. Je, ni njia zipi mbili ambazo Kanisa linaitwa kuwa wakala wa Mungu kupitia “ushahidi wake wa kitume”? Kwa nini ni muhimu sana kwamba Kanisa ulimwenguni lilinde ushuhuda na mafundisho ya Mitume kuhusu Kristo? 4. Kuna uhusiano gani kati ya Kanisa linalotumika kama mlinzi wa ushuhuda wa kitume, na kushiriki ushuhuda huo na waliopotea? Je, Kanisa linaweza kutimiza wito wake kama shahidi bila kufanya yote mawili? Kwa nini ndio au kwa nini hapana? 5. Kulingana na Maandiko, kwa nini ni lazima kwa Kanisa kudumisha na kuwa na bidii kwa ajili ya matendo mema? Matendo mema yanahusianaje hasa na kutangaza Ufalme ulimwenguni?
Sehemu ya 2
3
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
ukurasa 338 13
Made with FlippingBook Learn more on our blog