The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

/ 8 7

UFALME WA MUNGU

6. Huduma kwa maskini na wanyonge ina nafasi ya pekee katika maisha ya Kanisa – kwa nini? Kutaniko likikosa kutenda haki na huruma miongoni mwa maskini, kupuuza huko kunasema nini juu ya uwezo walo wa kutoa ushuhuda wake juu ya Ufalme mahali pake? 7. Ni katika maana gani Biblia inatuhakikishia kwamba kazi ambazo Yesu alifanya katika kudhihirisha Ufalme wa Mungu zitaendelea katika maisha na matendo ya Kanisa? 8. Ni kwa jinsi gani Roho Mtakatifu anafanya kazi katika kuthibitisha uhalali na nguvu za Neno la Mungu kupitia huduma ya Kanisa leo? Uhakikisho wetu unapaswa kuwa nini kwamba Roho Mtakatifu atafanya kazi katika nguvu za ufufuo wa Kristo tunapoenda ulimwenguni kuhubiri Injili? Somo hili linaangazia njia ambazo Kanisa la Yesu Kristo hutumika kama kituo (mahali au muktadha) ambapo Ufalme wa Mungu unaonyeshwa na kufunuliwa, pamoja na wakala wake, njia ambayo Ufalme wa Mungu unatolewa ushuhuda na kusonga mbele ulimwenguni. Ingawa Kanisa si Ufalme wenyewe wa Mungu, ni njia kuu ambayo Ufalme huo unadhihirishwa. Ufalme huunda Kanisa, kama ambavyo Mungu amefanya kazi kwa mamlaka katika nafsi ya Yesu ili kuzishinda nguvu za yule Mwovu, lakini Kanisa linaushuhudia Ufalme katika jumuiya yake na kupitia huduma yake. ³ Kanisa la Yesu Kristo ni mahali pa wokovu wa Mungu. Kupitia Kanisa, msamaha na upatanisho wa Ufalme unatangazwa kwa ulimwengu, na kutolewa kupitia huduma yake ya injili. Kama mlinzi wa Neno la Mungu, Kanisa linatangaza siri za upendo wa Mungu kwa waliopotea. ³ Kanisa ni mahali pa uwepo wa Roho Mtakatifu unaotia nguvu. Roho Mtakatifu ndiye arrabon , “malipo ya awali” na dhamana ya urithi ambao utafunuliwa katika Ujio wa Pili wa Yesu Kristo. Kanisa, kama makao ya Roho Mtakatifu, linaziishi baraka zote, matunda, na furaha inayohusishwa na huduma hai ya Roho kupitia washirika wa Kanisa. ³ Kanisa ni mahali pa uhai na nguvu za Ufalme. Katikati ya jamii ya waamini kuna uzoefu wa nguvu ya kujibiwa maombi, kuzaliwa upya na maisha mapya, utimilifu wa Mungu katika haki na amani, na nguvu za wakati ujao, yote katika jumuiya ya upendo.

MUUNGANIKO

Muhtasari wa Dhana Muhimu

3

Made with FlippingBook Learn more on our blog