The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
8 8 /
UFALME WA MUNGU
³ Katika mada hii ya Kanisa kama mahali pa Ufalme, tunaona kwamba Ufalme ni zawadi na kazi ya Kanisa. Kama zawadi, unadhihirishwa kupitia neema ya Mungu katika Roho. Kama kazi, Kanisa linaitwa kutoa ushuhuda wa utawala wa Mungu kwa njia ya maisha yake pamoja na mwingiliano wake na waliopotea duniani. ³ Kanisa sio tu eneo la Ufalme; pia ni wakala wa Ufalme, kwanza kabisa, katika ibada yake kwa Mwenyezi Mungu. Huu ndio utambulisho wa kimsingi wa Kanisa, Ufalme wa makuhani wa kifalme walioitwa kudhihirisha wema na matendo ya Mungu kupitia maisha na ibada yake. ³ Kanisa ni wakala wa Ufalme katika ushuhuda wake wa kitume. Kanisa linaitwa kutetea na kulinda ushuhuda wa kitume kuhusu Kristo, pamoja na kutoa ushuhuda kamili wa Injili ya Ufalme katikati ya waliopotea duniani kote. ³ Kanisa ni wakala wa Ufalme katika bidii yake na mwendelezo wa matendo mema, hasa katika matendo ya haki na huruma kwa ajili ya maskini. Yesu alipozindua na kutoa uhalali wa wito wake wa ufalme kwa njia ya huduma yake kwa maskini, ndivyo Kanisa linavyoendelea na ushuhuda huu wa ufalme kwa njia ya matendo yake kwa niaba ya maskini, ambao ni matajiri wa imani na walioitwa kuwa warithi wa Ufalme. ³ Kanisa ni wakala wa Mungu katika kuwa chombo cha Mungu kwa ishara na maajabu ya kinabii ambayo yanathibitisha huduma yake ya ufalme ulimwenguni. Kanisa katika zama hizi ni Kanisa Pambanaji (lililo vitani), likizikabili nguvu za giza kwa silaha za vita vya Mungu. Linapotoa ushuhuda wa utawala wa Mungu ulimwenguni, Kanisa linaweza kumtarajia Roho Mtakatifu kulithibitisha Neno lake kwa ishara za mabadiliko, haki, uponyaji, ukombozi, na wokovu. Sasa ni wakati wa wewe kujadili na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu jinsi Kanisa lilivyo mahali na wakala wa Ufalme. Maswali yako ni ya muhimu sana. Mawazo, maswali, na mashaka uliyo nayo sasa lazima yajadiliwe. Ukweli kuhusu Kanisa katika somo hili umejaa athari muhimu, na bila shaka sasa una maswali kuhusu umuhimu wa kweli hizi kwa kazi yako katika Kanisa, na kwa maisha na huduma yako. Maswali yafuatayo yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na muhimu zaidi.
3
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Wanafunzi
Made with FlippingBook Learn more on our blog