The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
9 2 /
UFALME WA MUNGU
Kiini cha mafundisho haya ni ili uweze kutafuta kuhusianisha kweli hizi na huduma yako mwenyewe kupitia kanisa lako. Jinsi Mungu anavyoweza kukutaka ubadilike au ubadilishe mbinu yako ya huduma kulingana na kweli hizi inategemea sana uwezo wako wa kusikia kile ambacho Roho Mtakatifu anakuambia kuhusu mahali ulipo, mahali uongozi wako wa kichungaji ulipo, mahali washirika wa kanisa lako walipo, na kile hasa ambacho Mungu anakuitia kufanya sasa hivi kuhusu kweli hizi, kama kipo. Panga kutumia muda mzuri wiki hii kutafakari juu ya wito wa Kanisa kama wakala wa kituo na wakala wa Ufalme, na ni kwa namna gani huduma yako na huduma ya kanisa lako zinaakisi wito huo. Unapofikiria na kujipanga kwa ajili ya kazi yako ya huduma kwa vitendo ili kukamilisha moduli hii, unaweza kuitumia kuzitendea kazi kweli hizi kwa njia ya vitendo. Utafute uso wa Mungu kwa ajili ya ufahamu zaidi, na urudi wiki ijayo ukiwa tayari kuwashirikisha wanafunzi wengine katika darasa lako maarifa ambayo umeyapata. Pengine kuna baadhi ya mahitaji maalum ambayo Roho Mtakatifu ameyaibua kupitia kujifunza na majadiliano yako katika somo hili juu ya Kanisa. Usisite kutafuta mtu wa kushirikiana naye katika maombi ambaye anaweza kushiriki kubeba mzigo ulionao na kuinua maombi yako mbele za Mungu. Bila shaka, Mkufunzi wako yuko tayari sana kutembea nawe katika hili, na viongozi wako wa kanisa, hasa mchungaji wako, wanaweza kuwa na ujuzi maalum wa kukusaidia kujibu maswali yoyote magumu yanayotokana na kutafakari kwako juu ya somo hili. Kuwa wazi kwa Mungu na umruhusu akuongoze jinsi anavyotaka.
Kuhusianisha somo na huduma
Ushauri na Maombi
3
MAZOEZI
1 Petro 2:9-10
Kukariri Maandiko
Ili kujiandaa kwa ajili ya darasa, tafadhali tembelea www.tumi.org/books ili kupata kazi ya kusoma ya wiki ijayo, au muulize mkufunzi wako.
Kazi ya usomaji
Kama kawaida unapaswa kuja na Fomu ya Ripoti ya Usomji ikiwa na muhtasari wako wa vitabu ulivyosoma kwa wiki. Pia, lazima uwe umechagua andiko kwa ajili ya kazi ya ufafanuzi ( eksejesia ), na uwasilishe mapendekezo yako kwa ajili ya kazi yako ya huduma kwa vitendo.
Kazi Nyinginezo
ukurasa 339 15
Made with FlippingBook Learn more on our blog