The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide
/ 9 7
UFALME WA MUNGU
Kukamilishwa kwa Utawala wa Mungu
SOMO LA 4
ukurasa 341 1
Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kushiriki katika mijadala, na kutendea kazi yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kufafanua eskatolojia na umuhimu wake kwa ufuasi wa Kikristo. • Kueleza kwa ufupi dhana ya kibiblia ya kifo, na kisha kujadili pamoja mafundisho ya Biblia kuhusu hali ya wafu. • kuzingatia Ujio wa Pili wa Yesu Kristo, ufufuo kutoka kwa wafu na hukumu ya mwisho, na kukamilishwa kwa Ufalme ambapo Mungu ni Yote-katika-yote. • Kukariri kifungu kinachohusiana na utimilifu wa utawala wa Mungu. Soma Ufunuo 5:1-14 . Katika mojawapo ya maono makuu zaidi kuhusu nyakati za mwisho katika maono ya Yohana ya kiapokaliptiki ya kitabu cha Ufunuo, tunasafirishwa hadi kwenye kiti cha enzi cha Mungu Mweza-Yote. Katika mkono wake wa kuume, Mwenye Nguvu alikuwa na kitabu, ambacho kufunguliwa kwacho kungeanzisha“mwanzo wa mwisho” wa programu ya Mungu ya ulimwengu ili kurejesha utawala wake katika ulimwengu wote. Katika tukio lililojaa uchungu na hasira, Yohana aliona kwamba hapakuwa na mtu yeyote mbinguni au duniani aliyestahili kukifungua kile kitabu, au hata kukitazama. Katika kukabiliana na tatizo hili, Yohana alisema kwamba alilia kwa uchungu na sana – katika ulimwengu wote hakuna aliyepatikana kuwa anastahili. Hatimaye, mmoja wa wazee alimwambia Mtume aliyekuwa analia, “Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba.” Yohana, anapogeukia tena tukio hilo la kutisha, anamwona Mwana-Kondoo amesimama katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne. Mwana-Kondoo huyu alionekana kuwa amechinjwa, alikuwa na pembe saba (akizungumza juu ya mamlaka yake) na macho saba (akizungumza juu ya Roho wa Mungu aliyetumwa duniani). Ni wakati huo ndipo wale wazee ishirini na wanne na wale wenye uhai wanne walipoimba wimbo wa kustahili kwa Mwana Ni nani Anayestahili Kukamilisha Utawala wa Mungu?
Malengo ya Somo
Ibada
4
ukurasa 342 2
Made with FlippingBook Learn more on our blog