The Kingdom of God, Swahili Mentor Guide

9 8 /

UFALME WA MUNGU

Kondoo kwa sababu alichinjwa na kumnunulia Mungu watu kutoka kila kabila, jamaa, taifa na lugha. Kwa maana halisi tukio hili kuu la kinabii linasisitiza moja ya imani za kimsingi za watakatifu na wahenga tangu mwanzo wa nyakati. Mungu pekee ndani ya Kristo ndiye anayestahili kutukuzwa, kupokea heshima, sifa, hekima na nguvu; kwa maana ni Yesu wa Nazareti pekee, Bwana aliyefufuka na kutawala juu ya wote, ambaye amejithibitisha kuwa anastahili kuleta utawala wa Mungu duniani. Hakuna kiasi cha vita, programu, juhudi za kibinadamu, teknolojia, hisani au wema wa kibinadamu kinachoweza kutuingiza katika utawala wa Mungu. Utimilifu wa Ufalme umekuwa ukitegemea nguvu na mapenzi ya Mwana-Kondoo aliyechinjwa. Kwa sababu hii, haiwezi kushindwa au kuzuiwa. Msifuni Mungu, kwa kuwa Ufalme unamtegemea Mwana, utakamilika, kwa kuwa anafanya mambo yote kuwa mema. Sifa zote ziwe kwa Mungu, Mwana-Kondoo peke yake ndiye anayestahili kuuleta utawala wa Mungu kwenye ukamilifu wake duniani! Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Mungu wa Milele, Baba yetu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, tunalitukuza jina lako kwa maana wewe peke yako ndiwe Mungu wa kweli wa mbingu na nchi. Mwanao, Bwana wetu Yesu Kristo, kati ya wengine wote wanaoitwa mabwana na miungu, ndiye pekee anayestahili kuleta utawala wako wa ufalme duniani kwa uzuri mkamilifu. Tunaliinua jina lako ndani yake, na tunaomba kwamba utupe hekima na nguvu za kukuheshimu na kukutukuza siku hiyo inapokaribia wakati Mwanao atakapofanya falme za ulimwengu kuwa milki yake. Katika jina la Yesu tunaomba. Amina.

Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi

4

Weka kando vitabu na madokezo yako, kusanya mawazo na tafakari zako, na ufanye jaribio la Somo la 3, Uvamizi wa Utawala wa Mungu .

Jaribio

Fanya mazoezi pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu kwa kutamka andiko la kukumbuka ulilopewa katika kipindi kilichopita: 1 Petro 2:9-10.

Mazoezi ya Kukariri Maandiko

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki iliyopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walikusudia kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji). Pia, ikiwa bado hujafanya hivyo,

Kazi za Kukusanya

Made with FlippingBook Learn more on our blog