The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

/ 5 7

UFALME WA MUNGU

4. Yesu kama Shujaa wa Mungu kwa njia ya msalaba.

III. Mwisho, Ufalme umezinduliwa katika Yesu kama Christus Victor , Yule anayeshinda kupitia ufufuo wake na kupaa kwake.

A. Ufunuo mkuu wa Ukristo, kulingana na Mtume Paulo, ni fundisho la ufufuo wa Kristo. Ikiwa Kristo hakufufuka, Paulo anasema:

1. Mahubiri ya Mitume hayakuwa na thamani.

2

2. Imani yetu katika ushuhuda wao ni bure.

3. Mitume ni walaghai, waongo, kwa vile wameonekana kuwa wamemwakilisha Mungu vibaya.

4. Imani yetu ni bure.

5. Bado tuko katika dhambi zetu.

6. Wakristo ambao wamelala wameangamia kabisa, wakiwa na matumaini katika maisha haya tu.

7. Hatimaye, sisi ni watu wa kuhurumiwa zaidi katika sayari hii.

8. Lakini, ashukuriwe Mungu! 1 Kor. 15:20.

Made with FlippingBook - Online catalogs