Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

1 0 2 /

THEOLOJIA YA KANISA

1. Kila mwamini mpya lazima ashirikiane moja kwa moja na kusanyiko la waamini, ambalo kwake linakuwa ni mwili wake na nyumba yake (Ebr. 10:24-25).

2. Kila mwamini, kama sehemu ya mwili huu, lazima ajue na kunyenyekea kwa viongozi wa Kanisa wanaomcha Mungu ambao wanatoa matunzo na mafunzo kwa ajili ya maisha na huduma zao (Ebr. 13:17).

a. Wanaongoza ibada na ukuaji wa Kanisa.

b. Wanahimiza ushuhudiaji wa Kanisa wa habari njema ya Kristo.

c. Wanaratibu kazi ya Kanisa ya huduma na utume ulimwenguni. (1) 1 Thes. 5:12-13 (2) 1 Tim. 5:17

3

III. Kipengele cha tatu cha Agizo Kuu ni kufundisha: Kanisa linatoa ushahidi kupitia mafundisho yake. Yesu alituamuru tuwafundishe wanafunzi wake kushika yote aliyowaamuru. Jitihada hii inalenga katika kuhubiri na kufundisha Neno la Mungu katika kusanyiko, na kupitia mafundisho hayo, kuwatayarisha waamini kuwa zaidi kama yeye na kufanya kazi yake ulimwenguni.

A. Kwanza, tumeitwa kushuhudia kwa kuhubiri na kufundisha Neno la Mungu katika kusanyiko la Kanisa.

1. Kati ya vipengele vyote muhimu katika ushuhuda wa Kanisa, lazima lijikite katika kuhubiri na kufundisha Neno la Mungu (2 Tim. 4:12).

Made with FlippingBook - Share PDF online