Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

1 0 4 /

THEOLOJIA YA KANISA

C. Tokeo mojawapo la kustaajabisha: washirika wa kanisa watashuhudia kuongezeka kwa kina na kufanana kwao na Kristo.

1. Lengo la ushuhuda wa Kanisa ni kwamba Kanisa likue katika idadi na ukomavu, na kuwafanya washirika waweze kumfanania Kristo zaidi na zaidi katika maisha yao binafsi na huduma yao kwa ulimwengu.

2. Lengo la shughuli za kiroho: kuzalishwa kwa maisha ya Kristo katika Kanisa. Kufanana na Kristo ndilo lengo la ufuasi wetu.

a. Lengo la Agizo Kuu: kufundisha waamini wapya kuzingatia na kufuata kila kitu ambacho Yesu ameamuru.

b. Mkazo huu kwa habari ya Kristo na Neno lake ni ufunguo wa ufuasi wa kibiblia katika Kanisa. Zaidi ya yote, lengo la wazi la maisha ya Mkristo ni kuwa kama Yesu katika maisha, kifo, na ufufuo wake.

3

c. Fil. 3:8

d. Gal. 4:19

e. Rum. 8:29

f. 2 Kor. 3:18

g. 1 Yoh. 3:2-3

Made with FlippingBook - Share PDF online