Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 1 0 5
THEOLOJIA YA KANISA
3. Hivyo basi, wito wa kushuhudia ni wito wa kuishi na kuakisi tabia na shauku ya Yesu Kristo katika maisha yetu, tukipendana sisi kwa sisi kama vile alivyotupenda sisi.
a. Sisi ni mwili wa Yesu pamoja katika ulimwengu huu (1 Kor. 12:27).
b. Kufanya wanafunzi ni kuchukua nira ya Kristo na kujifunza kwake (Mt. 11:28-30).
c. Tunapaswa kuonyesha wazi upendo ambao Kristo ametupenda (Yoh. 13:34-35).
4. Na tunapokwenda, kubatiza, na kufundisha, tunakuwa na uwezo mzuri zaidi wa kumwakilisha Yesu ulimwenguni na kuwafunulia waliopotea utukufu wake na utawala wake kupitia maneno, mwenendo na matendo yetu (2 Kor. 2:14-17).
3
Hitimisho
» Ushahidi wa Kanisa umefupishwa katika Agizo Kuu, ambalo lina vipengele vitatu tofauti vya wajibu wa mwili wa Kristo. » Kanisa linatoa ushuhuda kwa kwenda: Kanisa la Yesu Kristo limeitwa kwenda katika ulimwengu wote na kuhubiri Injili kwa waliopotea. » Kanisa linatoa ushuhuda kwa kubatiza: Kanisa limeitwa kubatiza waamini wapya katika Kristo, na kwa njia ya ubatizo, kuwajumuisha katika Kanisa la Kristo. » Kanisa linatoa ushuhuda kwa kufundisha: Kanisa la Yesu Kristo linawafundisha washirika wake kutii mambo yote ambayo Kristo ameamuru. Kwa kufanya hivyo, washirika wa Kanisa hukua hata kufikia ukomavu na kumfanania Kristo.
Made with FlippingBook - Share PDF online