Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

1 0 6 /

THEOLOJIA YA KANISA

Maswali yafuatayo yaliundwa ili kukusaidia kufanya marudio ya maudhui ya sehemu ya pili ya video. Ufahamu wa kina wa vipengele vya Agizo Kuu ni muhimu kwa wanaume na wanawake wa Kanisa kuelewa uhusiano wa Kanisa na ulimwengu, na wito wake wa kutangaza habari njema za wokovu kwa waliopotea. Vipengele vitatu vya kwenda, kubatiza, na kufundisha vinaunda kiini cha wito wetu wa pamoja wa kutoa ushuhuda kwa habari ya Kristo na Ufalme wake, na Kanisa limeitwa kuwa macho daima katika kufuatilia kila moja ya nyanja hizi tatu za maisha na huduma yake. Hakikisha kwamba unaelewa na unaweza kuelezea kanuni za msingi za kila kipengele, na unaweza kuhusisha kipengele hicho na jukumu la Kanisa kama shahidi. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko! 1. Nini asili ya kauli “Agizo Kuu,” na ni mambo gani matatu yaliyosisitizwa ndani yake ambayo yanatoa muhtasari wa wajibu wa ushuhuda wa Kanisa? 2. Nini maana ya sentensi katika Agizo Kuu, “Enendeni ulimwenguni mwote mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi?” Je, kuna uhusiano gani kati kufanya wanafunzi na uinjilisti na umisheni? 3. Upeo wa utume wa kwenda ulimwenguni kote ni wa aina gani, kwa maneno mengine, Yesu ametutaka tuwafanye kina nani kuwa wanafunzi, na tunapaswa kufanya hivyo wapi? 4. Ni nini asili ya ubatizo katika ushuhuda wa Kanisa? Je, kuna uhusiano gani kati ya ubatizo wa maji na imani inayookoa katika Yesu Kristo? Ikiwa ubatizo hautuokoi moja kwa moja, ni sababu zipi zinazomlazimu kila mwamini mpya kubatizwa? 5. Ubatizo unahusianaje na kuwaingiza waamini wapya katika kanisa? Kwa nini haiwezekani kwa mwamini kustawi ikiwa hatajumuishwa katika kusanyiko la waamini la mahali pamoja? 6. Muungano wetu na Kristo unaonyeshwaje kupitia ubatizo wetu? Kwa nini onyesho la muungano huu ni muhimu sana kwa ukuaji na ukomavu wa Kikristo? 7. Ni kwa jinsi gani maneno “kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi” yanajaza uelewa wetu wa Agizo Kuu? Nani amepewa kazi ya kutangaza na kufundisha Neno la Mungu katika Kanisa? 8. Mungu ameahidi nini kwa wale wanaolisha Neno la Mungu kupitia huduma ya kufundisha ya Kanisa? Je, lengo la kufanana na Kristo linahusiana vipi na lengo la kuyashika mafundisho ya Yesu katika Kanisa?

Sehemu ya 2

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

3

Made with FlippingBook - Share PDF online