Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 1 0 7

THEOLOJIA YA KANISA

9. Yesu anatuahidi nini katika Agizo Kuu kuhusu yeye mwenyewe wakati tunapotii agizo hili la kufanya wanafunzi duniani kote?

MUUNGANIKO

Somo hili linaangazia fundisho la uchaguzi jinsi linavyotumika kwa Yesu kama Mtumishi Mteule wa Mungu, na uchaguzi wa Mungu kwa Israeli na Kanisa kama mashahidi wa neema yake na kama mawakala wake ulimwenguni. Pia tuliangazia kwa undani vipengele mbalimbali vya Agizo Kuu (kwenda, kubatiza, na kufundisha) kama linavyohusiana na ushuhuda wa Kanisa ulimwenguni. Tena, umuhimu wa kiongozi wa Kikristo kuwa na uelewa na kufahamu kabisa mawazo haya uko wazi. Bila kuelewa jukumu la ushuhuda wa Kanisa, kiongozi wa Kikristo hataweza kuwafunza wengine kushuhudia kwa ufanisi au kuwa shahidi mwenye matokeo yeye mwenyewe. Hakikisha unaelewa mawazo ya kimsingi na Maandiko yanayohusiana na dhana hapa chini kwenye Kanisa kama shahidi. ³ Bwana Mungu, kama Mungu mkuu na mwenye mamlaka, amewaita na kuwachagua watu fulani kwa malengo na hadhi fulani. ³ Zaidi ya yote, Mungu amemchagua Yesu wa Nazareti kuwa Mtumishi wake Mteule, Anayeteseka. Katika Yeye, Mungu amechagua kuleta wokovu kwa wanadamu wote, kwa kila mtu anayeshikamana naye kwa imani katika kifo chake, kuzikwa na kufufuka kwake. ³ Mungu aliichagua Israeli kuwa chombo ambacho kwacho angemleta Masihi ulimwenguni, na ambacho kupitia hicho alitupatia picha ya wazi ya wokovu wake uliotolewa kwa Wayahudi na mataifa katika Yesu Kristo. ³ Waamini binafsi huchaguliwa “katika Kristo” kupitia muungano wao na ushirika pamoja naye. Mungu huwabariki watu wake wanapohusishwa na Kristo kupitia imani na utii wao. ³ Uchaguzi wa Mungu unategemea kusudi lake na neema yake kuu, iliyotolewa kwa wanyonge na dhaifu wa ulimwengu ili mtu yeyote asijisifu mbele zake. ³ Uchaguzi wa Mungu ni thabiti na umehakikishwa, kwa sababu hiyo tunaweza kuwa na uhakika wa wokovu wetu katika Yesu Kristo. ³ Jukumu ambalo Yesu alitoa kwa Kanisa lake kuwa shahidi wake limeelezwa kwa muhtasari katika Agizo Kuu.

Muhtasari wa Dhana Muhimu

ukurasa 254  12

3

Made with FlippingBook - Share PDF online