Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

1 0 8 /

THEOLOJIA YA KANISA

³ Utume huu unaweza kuelezewa kwa urahisi kulingana na vipengele vitatu muhimu, ambavyo vinaunda utume wa Kanisa ulimwenguni leo. ³ Kipengele cha kwanza ni kwamba Kanisa linatoa ushuhuda linapokwenda: Kanisa la Yesu Kristo limeitwa kutangaza Injili kwa waliopotea. ³ Kipengele cha pili ni kwamba Kanisa linatoa ushuhuda kwa njia ya ubatizo: Kanisa limeitwa kubatiza waamini wapya katika Kristo, yaani, kuwajumuisha kama washirika katika Kanisa. ³ Kipengele cha tatu ni kwamba Kanisa linatoa ushuhuda kupitia mafundisho yake: Kanisa la Yesu Kristo linafundisha washirika wake kushika mambo yote ambayo Kristo aliamuru, na hivyo kukua hadi kukomaa ndani yake. Sasa ni wakati wa wewe kujadili pamoja na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu asili ya fundisho la uchaguzi, na utiifu wetu kwa Agizo Kuu. Mada hizi zinawakilisha sehemu mbili za kina za mafundisho kuhusu ushuhuda wa Kanisa, na kupata kufahamu maana yake ni muhimu kwa ukomavu wako mwenyewe na pia uwezo wako wa kuwaleta wengine kwa Kristo na kuwaona wakikua hadi kukomaa ndani yake. Kuna maswali mengi magumu yanayohusishwa na mada hizi, hasa fundisho la uchaguzi, kwa hiyo unapaswa kuchukua muda wa kutosha kufikiria kwa uangalifu kupitia maswali yako na kutafuta majibu yaliyo wazi, ya kibiblia kwa maswali hayo. Je, una maswali gani hasa kwa kuzingatia yale ambayo umejifunza hivi punde? Labda baadhi ya maswali yaliyopo hapa chini yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na muhimu zaidi. * Je, Mungu huwachagua wengine waokolewe na wengine wapotee? Je, wazo lolote kama hili la Mungu kuchagua watu kwa ajili ya kupotea laweza kuwa halisi? * Ni katika maana gani Mungu huchagua watu mmoja-mmoja kwa ajili ya wokovu, au je, tunapaswa kuwekea maanani wazo la Mungu kuwachagua watu wake katika Kristo? * Kwa kuwa Israeli walishindwa kumwamini Kristo wakiwa kikundi, je, hilo linamaanisha kwamba Mungu amewaacha kama watu wake? Je, taifa la Israeli bado ni watu wa Mungu, na ikiwa ndivyo, kwa jinsi gani? * Ikiwa wokovu unatokana na Mungu kuonyesha rehema wala si matokeo ya jitihada zetu wenyewe, jukumu letu lilikuwa nini katika kumjia Yesu?

Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Wanafunzi

3

ukurasa 254  13

Made with FlippingBook - Share PDF online