Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
1 1 0 /
THEOLOJIA YA KANISA
Mungu ana upendeleo? Je, wale ambao hakuwachagua kabisa walikuwa na nafasi ya wokovu? Je, sisi si wanafiki tunapowaita watu waje kwa Yesu wakati tunajua kwamba baadhi yao hawawezi kamwe kumjia, haijalishi kwamba walitaka sana kumjia? Je, ungemsaidiaje mwanafunzi huyu mpendwa kutatua masuala haya?
Wote Wanainjilisha, ila Wachache ni Wainjilisti
Katika kikundi seli cha kanisa kilicholenga kujifunza kwa kina kuhusu umisheni, mjadala unazuka miongoni mwa washiriki kuhusu kama kila mtu anakusudiwa kutii Agizo Kuu. Wengine wanadai kwamba hata kama tungejitahidi na kujaribu kiasi gani, hatuwezi kamwe kuvuna nafsi za watu kama Billy Graham au Mtume Paulo. Watumishi hawa walijaliwa na Mungu kufanya kazi yao, ila sisi tumeitwa tu kushirikisha Habari Njema katika mzunguko wa marafiki na familia zetu. Wengine wanapinga, wakisema, Agizo Kuu ni neno la wakati kwa kila kizazi cha Wakristo. Waamini wote wanapaswa kutafuta njia ambazo wanapaswa kwenda, kubatiza, na kufundisha, kwa maana Yesu alituamuru kufanya hivyo. Hakuna mtu aliyeachwa kando; wote wanapaswa kuitikia Agizo. Je, unawezaje kushughulikia hoja hizi kinzani? Wakiwa wamekatishwa tamaa kabisa na kuchukizwa na watu wanaojifanya kuamini lakini si kweli, kanisa moja dogo la mtaa wenye makazi duni sasa linafundisha kwamba ili uokolewe ni lazima umkiri Yesu kuwa Bwana. Hili sio jambo jipya, kimsingi ndicho ambacho Warumi 10 inafundisha. Lakini, wamejaribu kulipeleka fundisho hilo kwenye kiwango kingine. Kwa sababu watu wengi sana wanadai kuwa wa Yesu lakini hawaonyeshi dalili yoyote ya kujitoa kwake, mchungaji ameanza kuwaambia watu wasiamini tu ukweli kuhusu ufufuo, bali wajitoe kibinafsi kuishi na kutii amri za Yesu ili waokolewe. Baadhi ya wazee wana wasiwasi; wanafikiri mchungaji anafundisha wokovu wa matendo ambao utawafukuza watu mbali na Bwana. Wengine wameyapokea mafundisho hayo kama njia mbadala inayohitajika na kuburudisha ikilinganishwa na mahubiri dhaifu na yasiyo na afya ambayo yanaonekana kuenea sana makanisani leo. Je, ungetoa maoni gani kuhusu mtanziko huu? Wokovu Unaosisitiza Ubwana wa Kristo
3
3
4
Made with FlippingBook - Share PDF online