Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 1 1 1
THEOLOJIA YA KANISA
Kwa msingi wa uchaguzi mkuu wa Mungu, Yesu wa Nazareti amefanyika kuwa Mtumishi Mteule wa Mungu, Yule ambaye kupitia kwake Mungu anaokoa ulimwengu, na ambaye ndani yake wote waliookolewa wanapata ukombozi wao. Israeli ni ishara na mtangulizi wa watu wateule wa Mungu, ambao kupitia kwao Masihi alikuja, ambaye alikufa, akafufuka, na anatawala kama Bwana mteule wa Mungu. Kanisa, ambalo ni mjumuiko wa Wayahudi na mataifa wote wanaoamini, ni watu ambao wameteuliwa na kuchaguliwa “katika Kristo,” yaani, wameungamanishwa na Kristo wanaposhikamana naye kwa imani. Agizo Kuu linatoa muhtasari wa jumla wa ushuhuda wa Kanisa kwa lengo la kufanya wanafunzi ulimwenguni, wenye sehemu tatu. Kanisa linatoa ushuhuda kwa kwenda na kufanya wanafunzi (kuinjilisha waliopotea ulimwenguni), kwa kubatiza (kujumuisha waamini wapya katika kusanyiko la waamini), na kwa kufundisha (kuwaagiza wanafunzi kufanya kila kitu ambacho Yesu anaamuru na hivyo kukua hadi kukomaa ndani yake). Ikiwa una nia ya kufuatilia baadhi ya mawazo yanayohusiana na mada zilizoletwa katika somo hili la Kanisa kama Shahidi , unaweza kujaribu vitabu hivi: Arn, Win, na Charles Arn. The Master’s Plan for Making Disciples. 2nd Edition. Grand Rapids: Baker Books, 1988 (1982). Coleman, Robert. The Master Plan of Evangelism. 30th Anniversary Edition with Study Guide by Roy J. Fish. Grand Rapids: Fleming H. Revell-Baker Books, 1993 (1963). Phillips, Keith. The Making of a Disciple. Old Tappan, New Jersey: Revell Books, 1981. Snyder, Howard. Kingdom, Church, and World: Biblical Themes for Today. Eugene, OR: Wipf and Stock Publishers, 2001 (1985). Ajabu ya kuchaguliwa na Mungu katika Kristo, na kuitwa na Mungu kuwa mfanya wanafunzi ni ukweli mtamu na unaogusa moyo sana kwetu kama waamini. Tumechaguliwa katika Kristo, tumeteuliwa, tumeitwa kwenda katika ulimwengu mzima kufanya wanafunzi, tukiwabatiza katika jina la Mungu wa Utatu, na kuwafundisha Neno takatifu la Kristo. Kweli hizi zina uhusiano wa moja kwa moja katika maisha na huduma yako kama mfuasi; huwezi kutimiza wajibu wako kama kiongozi ikiwa unashindwa kuthamini na kuelewa muungano wako na Mungu katika Kristo, na agizo la Yesu kwa Kanisa lake kutimiza kile kinachojulikana kama Agizo Kuu. Sasa ni wakati wako wa kutathmini jinsi ambavyo kweli hizi
Marudio ya Tasnifu ya Somo
Nyenzo na Bibliografia
3
Kuhusianisha Somo na Huduma
ukurasa 255 15
Made with FlippingBook - Share PDF online