Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 1 1 7
THEOLOJIA YA KANISA
Kanisa katika Kazi
SOMO LA 4
ukurasa 257 1
Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma kwako, kujifunza, majadiliano, na matumizi ya maudhui ya somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kuelezea hali na vipengele mbalimbali vya Kanisa, na kuweza kusema jinsi tunavyoweza kutambua jumuiya ya Kikristo halisi kupitia matendo na mtindo wa maisha wa Kanisa. • Kutambua alama za Kanisa kulingana na Kanuni ya Imani ya Nikea. • Kutambua vigezo na ufafanuzi wa Kanisa kulingana na mafundisho ya Matengenezo. • Kukariri msingi wa umoja wa kimafundisho kulingana na Kanuni ya Vincentian, ambayo ni mwongozo wa kusaidia kuelewa na kutathmini mapokeo na mafundisho yanayodai kuwa ya lazima kwa Wakristo. • Kuelezea tabia ya kazi za Kanisa ulimwenguni kwa kuchunguza picha mbalimbali za Kanisa zilizotajwa katika Agano Jipya. • Kufafanua juu ya asili ya Kanisa na kazi yake kupitia taswira (mfano) ya nyumba ya Mungu, mwili wa Kristo, na hekalu la Roho Mtakatifu, kupitia ubalozi wa Kanisa kama wakala wa Ufalme wa Mungu, pamoja na taswira ya “jeshi la Mungu,” kazi ya Kanisa kama kupigana vita katika vita vya Mwana-Kondoo. Soma 2 Wakorintho 5:18-21 . Kati ya taswira zote za Kanisa zenye mguso mkubwa na zinazotoa changamoto katika fahamu zetu, taswira ya kuwa balozi wa Bwana ni mojawapo ya picha tajiri zaidi na zenye ushawishi zaidi. Paulo anazungumza na Wakorintho kama balozi wa Kristo, ambaye anawakilisha maslahi, sera, na viongozi wa nchi ya mbali, na ambaye kazi yake muhimu ni kutekeleza amri na maagizo ya nchi yake. Katika Maandiko yote, Mungu anawatazama watu wake kama mali ya nchi tofauti, wakitazamia mji mpya na wa tofauti ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu mwenyewe. Watu hawa wa Mungu ni watu ambao uraia wao uko mbinguni, nao huweka shauku yao katika mambo yaliyo juu ambako Kristo ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Sisi ni wa Bwana; hatuna makao yadumuyo hapa. Sisi ni wageni na wapitaji, tukiwakilisha masilahi ya Ufalme wa Kujifunza Kumwakilisha Mungu
Malengo ya Somo
4
Ibada
ukurasa 257 2
Made with FlippingBook - Share PDF online