Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

1 1 8 /

THEOLOJIA YA KANISA

Mungu ambao, kimuujiza, umefunuliwa na kuzinduliwa katika Yesu Kristo kupita maisha na mateso yake. Kuwa Mkristo ni kuwa balozi wa Yesu Kristo, na kuwa kutaniko ni kuwa kituo cha ulinzi, ubalozi wa Ufalme wa Mungu katika jamii fulani. Jukumu letu ni kuiwakilisha “nchi ya asili” yetu, kupata maagizo kutoka kwa Waziri Mkuu wa mbinguni, na kuzitangazia mamlaka zilizo katika eneo hili Neno na mapenzi yake. Kuwa Mkristo ni kujifunza kuwakilisha wema, kuwa aina ya mwakilishi ambaye ni mwaminifu, mwazi, na asiyeyumbishwa. Je, wewe ni aina ya mwanamume au mwanamke anayewakilisha vyema maslahi na maagizo ya nchi yako? Je, Bwana aliye hai na Mkuu wa mji mpya ujao anaweza kukutegemea wewe kumtetea kwa uadilifu hapo ulipo? Simama kwa ajili ya Yesu unaposimama kwa ajili ya Ufalme ujao. Mungu wa Milele na Baba wa Bwana wetu Yesu, nakushukuru kwa wema wako, rehema na neema zako zinazotuwezesha kukuwakilisha ulimwenguni. Umeahidi kwamba Roho wako atatupa nguvu na kutuwezesha kutimiza mapenzi yako kwa ubora. Utupe nguvu na mwelekeo ili tuweze kusimama kwa ajili yako katika yote tunayosema na kufanya – katika nyumba zetu, kazi zetu, ujirani wetu na ndani ya makanisa yetu. Tunatamani kuwa aina ya wanafunzi unaowaona waaminifu, wale unaoweza kuwatumia kulitukuza jina lako katika ulimwengu usiokujua wala kukuheshimu. Ni Wewe Pekee unayeweza kutufanya kuwa aina ya wawakilishi wanaostahili kuwakilisha Jina Lako na Ufalme Wako. Utufanye kama Mwanao, ambaye alitimiza mapenzi yako kwa ukamilifu, na kujinyenyekeza ili Wewe upate kutukuzwa ndani yake. Tufanane na mfano wake, kwa ajili ya Jina lako, katika jina la Yesu, Amina. Baada ya kukiri na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (iliyopo kwenye viambatisho), omba maombi yafuatayo:

Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi

4

Weka kando daftari lako na nyenzo za kujifunzia, kusanya pamoja mawazo na tafakuri zako, kisha ufanye Jaribio la Somo la 3, Kanisa kama Shahidi.

Jaribio

Pitia pamoja na mwanafunzi mwenzako, andika na/au nukuu andiko la kukumbuka la kipindi kilichopita: Mathayo 28:18-20.

Mazoezi ya Kukariri Maandiko

Kusanya muhtasari wako wa kazi ya usomaji ya wiki iliyopita, yaani, jibu lako lenye maelezo machache kuhusu mambo muhimu uliyoyaona katika vitabu ulivyoelekezwa kusoma, yaani hoja kuu ambazo waandishi walitaka kuziwasilisha (taz. Fomu ya Ripoti ya Usomaji).

Kazi za Kukusanya

Made with FlippingBook - Share PDF online