Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

1 2 0 /

THEOLOJIA YA KANISA

Kanisa katika Kazi Sehemu ya 1

YALIYOMO

Mch. Dkt. Don L. Davis

Kihistoria, waamini wamebainisha na kusimamia vigezo fulani vya kuelewa hali na vipengele mbalimbali vya Kanisa, na jinsi tunavyoweza kutambua jumuiya ya Kikristo halisi kupitia matendo na mtindo wa maisha wa Kanisa. Vyanzo vitatu vimesaidia sana kuleta maana ya maono ya kibiblia ya Kanisa. Kwanza, alama au sifa za Kanisa kulingana na Kanuni ya Imani ya Nikea zinasisitiza kuhusu Kanisa kuwa moja, takatifu, la kitume na la ulimwengu wote. Ufafanuzi wa Kanisa kulingana na mafundisho ya Matengenezo ya Kanisa unasisitiza kuhubiriwa kwa Neno, uzingatiaji wa sakramenti na utaratibu sahihi wa nidhamu. Kuhusiana na ukweli wa mafundisho, kanuni ya Mtakatifu Vincent inasisitiza mambo ambayo yameaminiwa kila mahali, siku zote, na wote. Alama hizi zinasaidia katika kutambua matendo na mafundisho sahihi ya Kanisa. Malengo yetu ya sehemu hii ya kwanza ya Kanisa katika Kazi : • Kuelewa hali na vipengele mbalimbali vya Kanisa, na jinsi tunavyoweza kutambua jumuiya ya Kikristo ya kweli kupitia matendo na mtindo wa maisha wa Kanisa. • Tutaangalia alama za Kanisa kulingana na Kanuni ya Imani ya Nikea. • Tutachunguza kwa ufupi vigezo na ufafanuzi wa Kanisa kulingana na mafundisho ya Matengenezo ya Kanisa ( Reformation ). • Tutalitazama Kanisa kwa msingi wa Kanuni ya Vincent – mwongozo muhimu wa kuelewa na kutathmini mapokeo na mafundisho yanayodai kuwa ya muhimu kwa Wakristo.

Muhtasari wa Sehemu ya 1

4

Made with FlippingBook - Share PDF online