Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 1 2 1
THEOLOJIA YA KANISA
I. Alama za kiwango cha ki-kanuni: Kanisa kulingana na Kanuni ya Imani ya Nikea: “ Tunaamini katika Kanisa Moja, takatifu, katoliki na la mitume .” Kanuni ya Imani ya awali ya Nikea labda ilikuwa ni zao la mtaguso (yaani mkutano) wa kwanza wa ulimwenguni pote wa maaskofu wa Kikristo huko Nikea katika mkoa wa Bithinia (ambayo sasa ni Isnik, Uturuki) katika mwaka wa 325. Mafundisho ya mkutano huo wa kwanza yalithibitishwa na kupanuliwa katika mkutano wa baadaye mwaka wa 381. Mkutano huo wa awali ulitafuta kudhoofisha uzushi uitwao Uariani (ambao ulipinga uungu wa Yesu na kudai kuwa Yesu ni kiumbe kikuu cha Mungu). Mkutano huo pia ulikusudia kukanusha wazo kwamba Roho Mtakatifu si Mungu (yaani, si wa asili moja au kiini kimoja na Baba). Baraza la maaskofu 150 wa Kanisa la Mashariki lilikusanyika mnamo mwaka 381 huko Constantinople (Istanbul ya leo, Uturuki), ambapo walikiri tena kwamba Yesu ni Mungu kamili, na kupanua lugha ya mabaraza ya kwanza kujumuisha aya ya wazi ambayo ilionyesha uungu na kazi ya Roho Mtakatifu. Toleo la pili, lililopanuliwa la Kanuni ya Imani ya Nikea ya kwanza ya mwaka 325 linajulikana leo kama “Kanuni ya Imani ya Nikea.” Ikionekana kuwa mojawapo ya maungamo ya kwanza ya msingi ya imani ya Kikristo, Kanuni hii ya Imani inakubaliwa na mapokeo na madhehebu yote. Kuhusu Kanisa, Kanuni hii ya Imani inathibitisha “Tunaamini katika Kanisa Moja, Takatifu, Katoliki na la Mitume.” Sasa tuangalie kwa ufupi sifa (alama) hizi za Kanuni ya Imani kwa mtiririko huo.
Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video
4
A. Kwa kuanzia, kulingana na Kanuni ya Imani ya Nikea, Kanisa ni moja.
ukurasa 258 4
1. Ona jinsi umoja huu unavyoelezwa katika maombi ya Yesu ya ukuhani mkuu, Yoh. 17:20-23.
2. Ufahamu huu unathibitishwa tena na Paulo katika Waraka kwa Waefeso 4:4-6.
3. Mafundisho ya Yesu juu ya umoja: kundi moja la kondoo kwa ajili watu wake, Yoh. 10:14-16.
Made with FlippingBook - Share PDF online