Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

1 2 6 /

THEOLOJIA YA KANISA

3. Pia, sakramenti za kweli zilionekana kuwa tendo la imani hai, njia ya kutangaza hadharani kujitoa na uaminifu kwa kweli ya Mungu katika Yesu Kristo.

a. Ubatizo unathibitisha utambulisho wetu na Kristo katika kufa, kuzikwa, na kufufuka kwake, Rum. 6:3-4.

b. Meza ya Bwana inatoa ushuhuda wa utoshelevu wa kifo cha Yesu na kutazamia kwetu kurudi kwake hivi karibuni kwa ajili ya wokovu wetu wa mwisho.

4. Sakramenti za kweli lazima ziwe za manufaa ya kiroho na zenye kujenga kwa wale wanaozishiriki.

a. Ubatizo ni onyesho la nje la ungamo letu la imani na unatoa ushahidi kwa waamini wengine kuhusu kujitoa kwetu kuishi kama watumwa wa Yesu Kristo.

4

b. Tena, Meza ya Bwana inatoa neema na hakikisho tunapongojea kwa uthabiti katika tumaini la kurudi kwa Kristo.

5. Katika kuchunguza mapokeo mbalimbali ya Kikristo, ni wazi kwamba madhehebu yana maoni tofauti kuhusu sakramenti. Katika kujadili maswala hayo, maswali kadhaa muhimu huibuka:

a. Ni ibada zipi zilizopendekezwa ambazo ni sakramenti za kweli? Ingawa ubatizo na Meza ya Bwana hutambuliwa ulimwenguni pote kama sakramenti zilizoanzishwa na Yesu mwenyewe, mapokeo ya kimadhehebu yana maoni yanayokinzana kuhusu taratibu nyinginezo ambazo zinaweza kuchukuliwa kama sakramenti. Kwa mfano, Kanisa Katoliki linatambua baadhi ya sakramenti mbali na ubatizo na Meza ya Bwana au ekaristi, kutia ndani mambo kama vile kipaimara, ndoa, na ibada za mwisho.

Made with FlippingBook - Share PDF online