Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 1 2 7

THEOLOJIA YA KANISA

b. Je, sakramenti hutimiza nini hasa? Miongoni mwa Wakristo kuna kutokubaliana kuhusu kama sakramenti ni ishara tu, zinazoelekeza kwenye jambo fulani halisi la kiroho, au kama kweli Mungu humpa Mkristo neema na baraka za kipekee na za kutia nguvu zinazotokana na sakramenti husika. c. Ni nani mwenye sifa za kutoa sakramenti? Katika mapokeo na madhehebu fulani, ni viongozi waliowekwa maalum au wanaotambuliwa tu ndio wanaoruhusiwa kutoa sakramenti, wakati katika madhehebu mengine, mwamini yeyote katika ushirika mzuri anaweza kutoa sakramenti, kadiri fursa inavyoruhusu. d. Ni nani wana sifa za kupokea sakramenti? Takriban mapokeo yote ya Kikristo yanakubali kwamba ni waamini pekee ambao wanapaswa kupokea ubatizo na Meza ya Bwana, kwa maana ubatizo ni ishara ya utambulisho wa mtu na Kristo, na Meza ya Bwana inahusiana na muungano wa mwamini na Yesu Kristo na adhimisho la kifo cha Kristo kwa niaba ya mwamini.

4

C. Sifa ya mwisho ya Kanisa kwa mujibu wa Wana-Matengenezo ni “Mahali ambapo nidhamu imepangiliwa ipasavyo.” Hili linahusika na maisha na muundo wa kusanyiko chini ya uongozi wa wachungaji na wazee wao kwa njia ya Roho Mtakatifu.

1. Mpangilio sahihi wa nidhamu unazungumzia mfumo wa maisha miongoni mwa washirika wa kanisa. Aina zote za utaratibu zipo kwa ajili ya kulijenga Kanisa.

a. Yoh. 13:34-35

b. 1 Kor. 10:23-24

Made with FlippingBook - Share PDF online