Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 1 3 1

THEOLOJIA YA KANISA

Tafadhali chukua muda mwingi uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yametokana na video. Kuelewa jinsi ambavyo Kanisa limefafanua vigezo vya kusanyiko la kweli kunaweza kutusaidia katika kila hatua ya huduma yetu ndani ya Kanisa. Ingawa alama hizi za Kanuni ya Imani ya Nikea, Matengenezo ya Kanisa, na Kanuni ya Vincent hazijapangiliwa kwa uwazi kwa kufuata mtiririko fulani wa Maandiko mahususi, zote zinatokana na mafundisho ya wazi ya Yesu na mitume, na zinatupatia msaada wa thamani sana katika kuelewa asili ya Kanisa. Hakikisha, basi, kwamba unaelewa vipengele mbalimbali ambavyo vigezo hivi vinawakilisha. Kama kawaida, jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko! 1. Eleza kwa ufupi kila moja ya vigezo vinne vilivyotajwa katika Kanuni ya Imani ya Nikea kuhusu asili na kazi ya Kanisa. Ni kwa jinsi gani kila kigezo kimoja kinatusaidia kuelewa kazi ya Kanisa katika uhusiano wake na Mungu na ulimwengu? 2. Kwa nini tafsiri ya Kanisa kwa mujibu wa Kanuni ya Imani ya Nikea ni muhimu sana kwetu kuelewa na kutetea leo? 3. Kati ya vigezo vyote mbalimbali vinavyotajwa katika Kanuni ya Imani ya Nikea, je, unaamini kwamba kuna kigezo ambacho kinatawala zaidi ya vingine? Ikiwa ndivyo, ni kigezo kipi? 4. Je, Wanamatengenezo walielewaje asili ya kusanyiko la kweli la Kikristo – ni vigezo gani vitatu walivyotambua kuwa muhimu katika kutambua maisha ya kweli ya Kanisa? 5. Unapotafakari juu ya vigezo vitatu vya Kanisa kulingana na Wana Matengenezo, tunapaswa kuelewaje uhusiano ulipo kati ya vigezo hivyo? Je, vigezo hivi vinahusiana vipi na vigezo vya Kanisa kulingana na Kanuni ya Imani ya Nikea? 6. Eleza vizuri misingi ya Kanuni ya Vincent ya kutathmini ukweli wa madai ya kitheolojia kwa Kanisa. Kwa nini ingekuwa muhimu kwa Kanisa kuwa na kanuni kama hiyo ya kutathmini madai mbalimbali yanayokinzana kuhusu imani na utendaji wake? 7. Vigezo vya Kanuni ya Imani ya Nikea vya utume vinahusiana vipi na Kanuni ya Vincent? Kwa nini kanuni hizi mbili zinafaa kuhusianishwa kila mara ili kuchukulia kwa usahihi kile ambacho Kanisa limeamini katika historia? 8. Ni nani katika makutaniko yetu anayepaswa kuhusika zaidi na matumizi ya kanuni na vigezo hivi ndani ya makanisa yetu? Je, tunawezaje kuzitumia kwa ufanisi zaidi katika makanisa ya mijini?

Sehemu 1

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

ukurasa 262  9

4

Made with FlippingBook - Share PDF online