Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

1 3 0 /

THEOLOJIA YA KANISA

C. Hatimaye, kanuni hii inatoa muhtasari wa kanuni hizo kwa maneno haya: “Kile ambacho kimeaminiwa kila mahali, siku zote na watu wote”

1. Hiki ndicho kigezo cha ridhaa : madhehebu yote ya Kanisa yameshikilia msingi huu wa ukiri wa Imani.

2. Wakristo wote kila mara wamekiri msingi huu muhimu: uzushi, kwa ufafanuzi, ni ule unaobuni au kubadilisha maana ya kile ambacho “kimetolewa mara moja tu kwa watakatifu,” Yuda 3.

Katika sentensi rahisi ajabu tuna kanuni thabiti na ya uhakika ya kugundua mafundisho ya kweli na kuyatofautisha na mafundisho ya uongo kuhusu imani ya Kikristo. Tunaweza kuchukulia fundisho kuwa lenye mamlaka na la lazima kwa Kanisa kama linaweza kushinda mtihani wa kuwa “kile ambacho kimeaminiwa kila mahali, siku zote na watu wote.”

Hitimisho

4

Tumezingatia seti tatu za sifa za Kanisa:

» Kanuni ya Imani ya Nikea: Kanisa Moja, takatifu, la kitume na katoliki.

» Mafundisho ya Matengenezo ya Kanisa: Mahali ambapo Neno linahubiriwa ipasavyo, sakramenti zinatolewa ipasavyo, nidhamu imepangiliwa ipasavyo. » Kanuni ya Vincent: Kile ambacho kimeaminiwa kila mahali, siku zote, na wote.

Made with FlippingBook - Share PDF online