Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 1 2 9

THEOLOJIA YA KANISA

III. Sifa kuhusu mapokeo na Imani, au Kanuni ya Vincent: “Kile ambacho kimeaminiwa kila mahali, siku zote na watu wote.” Kanuni ya Vincent inatoa njia ambayo kwayo tunaweza kuamua kama mafundisho au matendo fulani yanaendana na fundisho la “Mapokeo Makuu” ya Kanisa moja la kweli la Yesu Kristo.

Mtakatifu Vincent wa Lerins, aliyekufa kabla ya mwaka 450 BK, alitoa ufafanuzi mzuri wa kiwango hiki katika kile kinachoitwa “Kanoni ya Vincent, kipimo cha usahihi chenye vipengele vitatu: quod ubique, quod semper, quod ab omnibus creditum est (kile ambacho kimeaminiwa kila mahali, siku zote na watu wote). Kwa jaribio hili lenye vipengele vitatu la uekumene, ukale, na ridhaa, Kanisa linaweza kupambanua kati ya mapokeo ya kweli na ya uongo. ~ Thomas C. Oden. Classical Pastoral Care . Toleo la 4. Grand Rapids: Baker Books, 1987. uk. 243.

A. Kanuni hii inathibitisha kwamba msingi wa mapokeo ya kweli ni “Kile ambacho kimeaminiwa kila mahali.”

1. Hiki ndicho kigezo cha kiekumene (yaani, kile ambacho kinaaminika kila mahali): Kanisa ni jumuiya ya imani ambayo kihistoria imeshikilia msingi wa maungamo yaliyojikita katika nafsi ya Kristo.

2. Imani ya Kikristo imejikita katika nafsi na kazi ya Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi, na msingi huu umeaminiwa na Wakristo wote tangu mwanzo.

4

B. Kisha, kanuni hii inapanua kiwango ili kujumuisha “Kile ambacho kimeaminiwa kila mahali siku zote.”

1. Hiki ndicho kigezo cha ukale (yaani, kile ambacho kimekuwepo tangu mwanzo): Kanisa limeshikilia msingi huu wa ukweli wa maungamo uliowekwa katika Yesu katika vizazi vyote, kuanzia kizazi cha mitume.

2. Wakristo wamekiri daima msingi muhimu, tangu mwanzo: wokovu wa Mungu katika Kristo ni msingi ambao juu yake imani na matendo yote ya Kikristo yanajengwa.

Made with FlippingBook - Share PDF online