Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

1 3 4 /

THEOLOJIA YA KANISA

2. Kama makao ya Mungu Mwenyewe, washirika wa Kanisa lazima kibinafsi wafuate mitindo ya maisha inayoakisi usafi wa Mungu, maana hii ndiyo kazi yetu kuu kama watu wa Mungu, 2 Kor. 6:16-7:1.

Picha hizi za Kanisa katika Agano Jipya, yaani familia ya Mungu, mwili wa Kristo, na hekalu la Roho, zinatuwezesha kuelewa kazi yetu ya kuakisi ubora wa Mungu mwenyewe. Kabla ya jambo lingine lolote, tunapaswa kuonyesha umoja wetu katika utume, ushirikiano wetu wa pamoja katika kufanya mapenzi ya Mungu, na kufuatilia kwetu utakatifu katika matendo na shughuli zetu. II. Kanisa linapaswa kuakisi utawala wa haki wa Ufalme kupitia kazi zetu za uhuru, ukamilifu, na haki, kama mabalozi wa Kristo. 2 Kor. 5:18-21 – Tunapaswa kuishi na kufanya kazi kama mabalozi wa Kristo, tukiwakilisha Ufalme wa Kristo na kuwaalika watu wote wapatanishwe na Mungu. Tuko katika ulimwengu huu, lakini si wa ulimwengu huu. Fil. 3:20-21 – Sisi ni raia wa mbinguni kwa njia ya imani katika Yesu Kristo. 1 Pet. 2:16 – Sisi ni wageni na wapitaji duniani, tukizunguka kuelekea makao yetu ya kweli, Yerusalemu Mpya. Kama mabalozi, tunashiriki katika kazi zinazofunua uhuru, ukamilifu, na haki ya Ufalme.

4

A. Kwanza, kama mabalozi wa Kristo, tunafanya kazi kudhihirisha uhuru wa Ufalme.

1. Huduma ya Yesu na Isaya 61: Mwaka wa Yubile, huduma yake ya kutangaza habari njema kwa maskini, uhuru kwa wafungwa, na kupata kuona tena kwa vipofu.

2. Msisitizo huo huo juu ya uhuru ndio msingi wa kazi nyingi za watu wa Mungu katika Agano la Kale, Kum. 15:12-15.

Made with FlippingBook - Share PDF online