Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 1 3 5
THEOLOJIA YA KANISA
3. Kwa hiyo, kama watu tuliowekwa huru na Mungu, tunapaswa kusimama dhidi ya mambo yote yanayozaa uonevu na utumwa, hasa yale mazoea potovu ya kiroho ambayo yanaakisi mapenzi ya shetani na dhamira yake ya kuharibu watu na kuwafanya watumwa. Kama mawakala wa Mungu, tunapaswa kufanya kazi zinazolenga katika ukombozi wa yatima na waliodhulumiwa, Zab. 10:15-18.
4. Kama mabalozi wa Ufalme tunapaswa kuwekeza katika kazi zinazopambania uhuru na ukombozi kutoka katika uonevu na utumwa wa uovu, iwe ni wa kiuchumi, kitamaduni, kisiasa, au kijamii.
a. Kama watetezi wa uhuru wa Kristo ni lazima tujizatiti katika kuwa na mwitikio wenye ubunifu dhidi ya utumwa, na kuthibitisha thamani ya asili ya wanadamu kama ya pekee na maalum, iliyofanywa kwa mfano wa Mungu, inayostahili kuthaminiwa na kutunzwa.
b. Ni lazima tujitahidi kuunga mkono watu binafsi na shughuli zinazoendana na agizo la Mungu la amani na uhuru miongoni mwa wanadamu, Mit. 24:11-12.
4
B. Pili, kama mabalozi wa Kristo, tunashiriki katika kazi za kudhihirisha ukamilifu wa Ufalme.
1. Bila shaka, Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu ni Mungu anayetamani sana kuleta uzima kwa waliosetwa na kudharauliwa katika ulimwengu, Zab. 146.
2. Kama mabalozi wa Kristo, wale ambao wamefanywa kuwa wazima katika Kristo, sasa tunasimama dhidi ya mambo yote ambayo yanaleta mafarakano, magonjwa, madhaifu, mateso na taabu kwa wanadamu wengine kila mahali.
Made with FlippingBook - Share PDF online