Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

1 4 2 /

THEOLOJIA YA KANISA

Maswali yafuatayo yaliundwa ili kukusaidia kufanya marudio ya maudhui ya sehemu ya pili ya video. Kufahamu asili na kazi ya Kanisa kupitia picha za kibiblia ni njia iliyothibitishwa na thabiti ya kutambua kazi ya Kanisa. Somo letu limejikita kwenye mfululizo wa picha zinazoangazia uhusiano wa karibu ambao Kanisa linao na Bwana mwenyewe, na ulimwengu, na adui wa Kristo, Ibilisi. Kila taswira inatupatia wazo zuri la kitheolojia la kile ambacho Kanisa linapaswa kufanya kama watu wa Mungu mwenyewe ulimwenguni. Hivyo basi, jibu maswali haya kwa uangalifu, ukizingatia jinsi yanavyotusaidia kuelewa vyema kile ambacho Kanisa linapaswa kuwa na kufanya. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi na inapowezekana, utumie Maandiko! 1. Kwa nini ni jambo halali kuelewa asili na kazi ya Kanisa kupitia taswira za Kanisa katika Agano Jipya? Ni aina gani ya mambo tunapaswa kufahamu tunaposhiriki katika aina hii ya elimu? 2. Ni mipaka gani (ikiwa ipo) inapaswa kuwekwa katika kufanya utafiti kwa njia hii, yaani, kupitia sitiari (lugha ya picha, mifano) na mlinganisho? Ni kwa jinsi gani tunaweza kutumia njia hii vizuri zaidi ili kufaidi kikamilifu yale ambayo Roho anatufundisha kupitia mlinganisho huu kuhusu utambulisho wa Kanisa? 3. Je, tunajifunza nini kuhusu kazi ya Kanisa kupitia mfano wa kibiblia wa Kanisa kama «nyumba» au «familia» ya Mungu? Je, hii inatusaidiaje kuelewa kile ambacho Kanisa linapaswa kufanya katika mahusiano yake, hasa miongoni mwa washirika wake? 4. Je, mfano wa “mwili wa Kristo” unatusaidiaje kuelewa kile ambacho Kanisa linapaswa kufanya ulimwenguni? 5. Tunajifunza nini kuhusu kazi ya Kanisa ulimwenguni kupitia wazo la Kanisa kama “hekalu la Roho Mtakatifu?” Je, taswira hii inafanya nini kutufundisha kuhusu jukumu la Kanisa ulimwenguni? 6. Eleza baadhi ya majukumu, wajibu, na kazi mbalimbali zinayoambatana na wazo la kuwa balozi. Je, picha hii hai inatusaidiaje kuelewa kile ambacho Kanisa linapaswa kufanya ulimwenguni, kama mwakilishi wa Yesu Kristo? 7. Je, ni ufahamu gani tunaopata kuhusu asili ya kazi ya Kanisa kupitia taswira ya Kanisa kama askari au jeshi la Mungu? Je, picha hii inawezaje kutusaidia kuwaandaa washirika wetu, kupanga na kutumia rasilimali zetu, na kupangilia shughuli zetu kulingana na maana ya picha hii?

Sehemu 2

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

ukurasa 264  12

4

Made with FlippingBook - Share PDF online