Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

1 4 6 /

THEOLOJIA YA KANISA

Wakristo Hawafanyi Vita

Kikundi cha vijana kanisani kimekuwa kikijifunza masomo ya Biblia yanayosisitiza vita vya kiroho na utambulisho wetu kama askari wa Mungu. Kutokana na hilo, baadhi ya wazazi wameanza kuwa na wasiwasi kuhusu lugha na maneno hayo kuhusu vita na taswira nzima ya kivita, na jinsi inavyoweza kuathiri vibaya watoto katika kundi la vijana. Mifano ya vita vya msituni, mabomu, mapanga, ngao, nguvu za giza, na kadhalika zimeibua hofu kwa baadhi ya wazazi, ambao wanajiuliza kama tatizo ni kwamba mchungaji kijana wa kikundi hiki cha vijana anachukulia vibaya usomaji wake wa mifano ya Biblia kuhusu Kanisa kama jeshi la Mungu. Ni miongozo gani tunapaswa kutumia ili kutambua endapo tumeenda mbali sana katika matumizi yetu ya mifano na taswira katika Biblia katika jitihada za kupambanua mafundisho yetu, utambulisho wetu, na shughuli zetu katika Kanisa? Toa jibu sahihi. Alipokuwa akishirikishana imani yake na mtu wa dini ya Yunitariani kazini kwao, Ralph alipigwa na butwaa. Alipokuwa akizungumzia upendo wa Mungu katika Yesu Kristo, mtu huyu aliyekuwa akizungumza naye alisema kwa ghafla, “Wengi wenu katika makanisa ya aina yenu mmechanganyikiwa kabisa. Mnazungumza kuhusu Mungu, Yesu, na Roho Mtakatifu kama Utatu. Nimesoma Biblia nzima angalau mara sita, na sijawahi kupata hata neno lolote linalotajwa katika Biblia kuhusu Utatu. Unadai kuwa unaielewa Biblia, lakini sioni Utatu katika Biblia!” Je, unawezaje kutumia vigezo vya Kanuni ya Imani ya Nikea, vigezo vya mafundisho ya Wana-Matengenezo ya Kanisa, au Kanuni ya Vincent kumsaidia kuelewa kwa nini maoni ya Kanisa kuhusu Utatu si tu ya kibiblia bali pia yanakubaliana na mapokeo ya Kanisa? Baada ya kusikiliza mfululizo wa masomo ya mchungaji kuhusu Kanisa kama balozi wa Kristo duniani, mmoja wa wanasheria vijana katika kanisa hilo ambaye alikuwa anafikiria kugombea Udiwani wa Jiji anafikiria kuondoa jina lake na kuachana na dhamira ya kutaka kupigiwa kura. Akiwa ameshawishiwa kwa nguvu na mahubiri ya mchungaji kwamba Wakristo ni wageni na wasafiri katika ulimwengu huu, mgombea huyu kijana anajiuliza ikiwa kushiriki katika nyadhifa za serikali za kiulimwengu ni kujiingiza sana katika mambo ya ulimwengu. Maana kama sisi tupo katika ulimwenguni lakini si wa ulimwengu, labda kugombea nafasi ya kisiasa na kukaa kwenye Halmashauri ya Jiji ni tendo la kidunia sana. Je, iwapo mgombea huyu angekuuliza maoni yako, ungemshauri nini? Sioni Utatu katika Biblia Sisi Sio wa Ulimwengu Huu

2

3

4

4

Made with FlippingBook - Share PDF online