Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 1 8 7

THEOLOJIA YA KANISA

Theolojia ya Kanisa (muendelezo)

c. Kuanzisha makanisa miongoni mwa wale ambao hawajafikiwa na Injili (Mt. 16:18; 28:19; Mdo 2:41-42; 16:5; 2 Kor. 11:28; Ebr. 12:22-23). d. Kuonyesha ubora wa Ufalme wa Kristo kwa kutokeza uhuru, ukamilifu, na haki katika Jina lake (Isa. 53:5; Mika 6:8; Mt. 5:16; 12:18-20; Lk. 4:18-19; Yoh. 8:34-36; 1 Pet. 3:11). 4. Kutenda kama jamii ya kinabii a. Kulitamka Neno la Mungu kwa wale walio katika mazingira ya makosa, kuchanganyikiwa, na dhambi (2 Kor. 4:2; Ebr. 4:12; Yak. 5:20; Tito 2:15). b. Kuzungumza kwa ajili ya wale ambao hawawezi kujitetea ili haki ilindwe (Mit. 31:8-9). c. Kutangaza hukumu dhidi ya dhambi za namna zote (Rum. 2:5; Gal. 6:7-8; 1 Pet. 4:17). d. Kutangaza matumaini pale ambapo dhambi imezaa kukata tamaa (Yer. 32:17; 2 The.2:16; Ebr. 10:22-23; 1 Pet. 1:3-5). e. Kutangaza kurudi kwa Yesu, uharaka wa saa yake, na ukweli kwamba hivi punde kila goti litapigwa na kila ulimi utakiri kwamba Yesu ni Bwana kwa utukufu wa Mungu Baba (Mt. 25:1-13; Flp. 2:10-11; 2 Tim. 4:1, Tito 2:12-13).

Kanisa Ni Jamii Moja Ambamo Sakramenti Zinasimamiwa Ipasavyo

IV. Jamii ya Ibada

A. Kanisa linatambua kwamba kuabudu ndilo kusudi la msingi la uumbaji wote. 1. Mwabudu huabudu, kusifu, na kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyo na kwa matendo yake, akimpa thamani na utukufu unaomstahili. Ibada hii inaelekezwa kwa:

Made with FlippingBook - Share PDF online