Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

1 8 8 /

THEOLOJIA YA KANISA

Theolojia ya Kanisa (muendelezo)

a. Baba Mwenyezi ambaye ndiye Muumba wa vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. b. Mwana ambaye kwa kuvaa mwili, kifo, na ufufuo wake alileta wokovu na ambaye sasa anatukuzwa akiwa katika mkono wa kuume wa Baba. c. Roho ambaye ni Bwana na Mpaji wa Uzima. 2. Kuabudu ndilo kusudi kuu la mbingu na dunia inayoonekana, na maisha yote ndani yake (Zab. 148-150; Lk. 19:37-40; Rum. 11:36; Ufu. 4:11; 15:3-4). 3. Kuabudu ni shughuli kuu ya majeshi ya malaika wanaomwadhimishwa Mungu mbele zake (Isa. 6; Ufu. 5). 4. Ibada ndiyo wito mkuu wa “jamii ya watakatifu,” Wakristo wote wa kweli, walio hai na wafu, wanaotafuta kumtukuza Mungu katika mambo yote (Zab. 29:2; Rum. 12:1-2; 1 Kor. 10:31; Kol. 3:17). B. Kanisa hutoa ibada inayokubalika kwa Mungu. Hii inamaanisha: 1. Waabudu wameikana miungu yote ya uongo au mifumo ya imani ambayo inadai utii wao na wameingia katika agano la kumtumikia na kumwabudu Mungu mmoja wa kweli (Kut. 34:14; 1 The.1:9-10). 2. Waabudu wanaabudu: a. Katika Roho – kama watu waliozaliwa upya ambao, kupitia imani iokoayo katika Yesu Kristo, wamejazwa na Roho Mtakatifu na wanaishi chini ya uongozi wake. b. Katika Kweli – kumwelewa Mungu jinsi anavyofunuliwa katika Maandiko na kuabudu kulingana na mafundisho ya Neno. c. Katika Utakatifu – kuishi maisha ambayo yanaakisi kujitoa kwao kwa kweli kumtumikia Mungu Aliye Hai.

C. Kanisa linaabudu kama ukuhani wa kifalme, linatoa dhabihu za sifa kwa Mungu kwa moyo wote na kutumia rasilimali zake zote za uumbaji kumwabudu kwa ubora.

Made with FlippingBook - Share PDF online