Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 1 8 9

THEOLOJIA YA KANISA

Theolojia ya Kanisa (muendelezo)

1. Kanisa la Kristo ni watu wanaoabudu, si mahali pa ibada. 2. Kusanyiko lote linamtumikia Bwana, kila mmoja akichangia wimbo, neno, ushuhuda, maombi, n.k. kulingana na karama na uwezo wake (1Kor. 14:26). 3. Kanisa linaabudu kwa upeo kamili wa hisia za kibinadamu, akili, na ubunifu: a. Kujieleza kwa Mwili – kuinua mikono, kucheza, kupiga magoti, kuinama, nk. b. Ushirikiano wa kiakili – kujitahidi kuelewa asili ya Mungu na kazi yake. c. Kujieleza kwa sanaa – kupitia muziki na sanaa zingine za ubunifu. d. Onyesho la kisherehe – Kanisa hucheza katika uwepo wa Mungu (Mithali 8:30-31) likifurahia “pumziko la Sabato” kupitia maadhimisho, sherehe na sifa. 4. Kanisa huabudu kiliturujia kwa kuigiza kwa pamoja hadithi ya Mungu na watu wake. a. Kanisa linatangaza na kujumuisha mchezo wa kuigiza wa tendo la ukombozi la Mungu katika liturujia, mapokeo, na taratibu za ibada zake. b. Kanisa, kama watu wa agano Israeli, linapangilia maisha yake kwa kuzingatia sherehe ya Meza ya Bwana na Ubatizo ambavyo vinaigiza hadithi ya wokovu wa Mungu (Kum. 16:3; Mt. 28:19; Rum. 6:4; 1 Kor. 11:23-26). c. Kanisa linakumbuka ibada na huduma ya watakatifu katika vizazi vyote, likijifunza kutokana na uzoefu wao na Roho wa Mungu (Kum. 32:7; Zab. 77:10-12; 143:5; Isa. 46:9; Ebr. 11). 5. Kanisa linaabudu kwa uhuru: a. Kushiriki kila mara namna mpya na maonyesho mapya ya ibada ambayo yanampa Mungu heshima na kuruhusu watu wake kumfurahia tena (Zab. 33:3; 40:3; 96:1; 149:1; Isa. 42:9-10; Lk. 5:38; Ufu. 5:9).

Made with FlippingBook - Share PDF online