Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 1 9 9
THEOLOJIA YA KANISA
Theolojia ya Kanisa (muendelezo)
a. Tunawajibika kwa Mungu kwa namna tunavyosimamia yale tuliyokabidhiwa kibinafsi na kwa pamoja kama ushirika (Mt. 25:14-30). b. Pesa inapaswa kusimamiwa kwa njia ambayo hazina zinawekwa mbinguni (Mt. 6:19-21; Lk. 12:32-34; Lk. 16:1-15; 1 Tim. 6:17 19). c. Kuutafuta kwanza Ufalme wa Mungu ndicho kipimo ambacho kwa hicho uwakili wetu unapimwa, na msingi wa kukabidhiwa zaidi (Mt. 6:33). 2. Uwakili ufaao unapaswa kuchangia katika kuweka usawa na kushirikishana mema (2 Kor. 8:13-15). 3. Uchoyo ni dalili ya uwakili usio wa uaminifu na kumkataa Mungu kama mmiliki na mtoaji wa vitu vyote (Lk. 12:15; Lk. 16:13; Efe. 5:5; Kol. 3:5; 1 Pet. 5:2). E. Haki ni lengo kuu la Kanisa linapomtumikia Mungu na wengine. 1. Kutenda haki ni sehemu muhimu ya kutimiza utumishi wetu kwa Mungu (Kum. 16:20; 27:19; Zab. 33:5; 106:3; Mit. 28:5; Mik. 6:8; Mt. 23:23). 2. Haki ni sifa ya mtumishi mwadilifu lakini haipo kwa wanafiki na wasio haki (Mit. 29:7; Isa. 1:17; 58:1-14; Mt. 12:18-20; Lk. 11:42).
Made with FlippingBook - Share PDF online