Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 2 1 7
THEOLOJIA YA KANISA
Ufunuo Kivuli wa Kanisa katika Mpango wa Mungu
MAELEZO YA MKUFUNZI 1
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi wa Somo la 1, Ufunuo Kivuli wa Kanisa katika Mpango wa Mungu. Lengo la jumla la moduli hii ya Theolojia ya Kanisa ni kuzingatia ukweli muhimu wa jinsi Kanisa lilivyofunuliwa kwa njia ya kivuli katika kusudi kuu la Mungu la wokovu. Tangu mwanzo Mungu aliazimia kujiletea utukufu kwa kuwavuta kwake jamii ya wanadamu iliyofanywa upya kupitia agano ambalo alilifanya na Abrahamu. Mpango huu wa ajabu haukujumuisha tu wale wa ukoo wa kimwili wa Ibrahimu ambao wangemwamini Kristo, lakini pia ulijumuisha Mataifa ambao wangemjia kwa imani. Siri hii kuu ya kujumuishwa kwa Mataifa katika Kristo Yesu imefunuliwa katika enzi na wakati huu kupitia mitume na manabii. Zaidi ya hayo, lengo la somo hili ni kueleza kwa undani nia ya Mungu ya kuifanya jamii hii mpya ya wanadamu kuwa Watu wake wa pekee, Laos wa Mungu. Kwa hiyo, wokovu unaungamanishwa kikamilifu na nafasi ya mtu katika jamii hii ya watu wa Mungu, umefungamanishwa kwa karibu na unahusiana na ushiriki wa mtu katika Kanisa. Moduli hii ni muhimu kwa ajili ya kuwaendeleza viongozi kwa kuwa inaweka ndani ya akili na mioyo ya wanafunzi jukumu kuu la Kanisa katika mpango wa wokovu wa Mungu. Malengo haya yameelezwa kwa uwazi katika kipengele cha Malengo ya Somo , na unapaswa kuyasisitiza katika somo lote, wakati wa majadiliano na muda wote uwapo pamoja na wanafunzi. Kadiri unavyoweza kuangazia malengo katika kipindi chote cha darasa, ndivyo unavyotengeneza uwezekano mkubwa zaidi kwa wanafunzi kuelewa na kufahamu ukubwa wa malengo haya. Elekeza mkazo wa kipindi chote cha mafunzo katika kufikia malengo haya. Hakikisha kwamba unahusianisha vipengele vyote vya uwasilishaji wa somo na ushiriki wa wanafunzi na malengo. Usisite kujadili malengo haya kwa ufupi kabla ya kuingia katika kipindi. Vuta usikivu wawanafunzi kuelekea malengo haya, kwani, kiuhalisia, hiki ndicho kiini cha dhumuni lako la kielimu unapofundisha vipindi vya somo hili. Kila kitu kinachojadiliwa na kufanyika kinapaswa kulenga kwenye malengo haya. Tafuta njia za kuyasisitiza haya kila wakati, kuyakazia na kuyarudia tena na tena unapoendelea na somo. Kadiri unavyopata nafasi zaidi ya kuzingatia malengo, ndivyo inavyokuwa bora zaidi. Kwa mara nyingine tena, tunachotafuta kwa ujumla ni kwamba wanafunzi wapate kufahamu jinsi ambavyo Mungu alitoa muhtasari makini wa umuhimu wa Kanisa katika kila awamu ya kazi yake katika historia, katika kazi yake na watu wake, na hasa katika kazi yake ya wokovu.
1 Ukurasa 15 Utangulizi wa Somo
2 Ukurasa 15 Malengo ya Somo
Made with FlippingBook - Share PDF online