Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
2 1 8 /
THEOLOJIA YA KANISA
Ibada hii inalenga katika utambulisho wa Kanisa kama taifa takatifu la Mungu mwenyewe. Ona msisitizo hapa wa jinsi Kanisa linavyoakisi na kuonyesha utukufu na kiwango cha Mungu na Ufalme wake, au, angalau, linavyopaswa kutamani kuonyesha ukuu huu katika maisha na kazi yake. Bila shaka, ni tatizo la kawaida miongoni mwa wanaume na wanawake wa Kanisa kuwa na mawazo duni na ya aibu kuhusu Kanisa. Na si ajabu, kwa kuzingatia ukweli kwamba Kanisa limekuwa na sehemu yake ya matendo yenye kuhuzunisha ya dhambi, uchoyo, na udunia. Makanisa hasa wakati mwingine hayaakisi utukufu wa Kanisa moja, la kweli, na mara nyingi wanafunzi wetu wanaweza kuangukia kwenye mazoea ya kulikemea na kulikataa Kanisa inapobidi. Misemo kama vile “ukanisa” ni ya dharau, na mara nyingi watu wanaweza kutoa maoni ya kukashfu na yenye chuki kuhusu matendo na mazoea ya makusanyiko ambayo maisha yao hayaakisi heshima, utukufu na utambulisho wa asili ya Mungu. Kusudi la ibada hii ni kuanza mara moja kwa mtazamo wa wazi kwamba Mwenyezi Mungu amelichagua Kanisa, na kwamba Kanisa, kama watu wake wateule, lina jukumu muhimu na la kipekee katika kumwakilisha Mungu na masilahi yake ulimwenguni leo. Hakika, kuwa sehemu ya Kanisa ni kuwa sehemu ya jumuiya ya Mungu, na kupewa nafasi ya juu na wito wa kumfunua Yeye na makusudi yake kwa ulimwengu kwa njia ya maneno na matendo. Hakuna kutaniko moja linaloweza kudai kutimiza kusudi hili kikamilifu, lakini haya ndiyo matamanio yetu ya pamoja na shauku yetu kubwa zaidi. Maombi yaliyomo katika masomo haya yamekusudiwa kusisitizwa, si tu kama utangulizi rasmi wa somo na dhana zake, bali kama mwaliko wa kutoka moyoni kwa Mungu kuja katikati ya wanafunzi na kufanya kazi ambayo Roho Mtakatifu pekee anaweza. Yesu ameweka wazi kwamba huduma ya kufundisha ya Roho Mtakatifu ni huduma kuu na ya uzima. Yohana 16:13 – Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Chukua muda wa maombi kwa umakini, kwani kwa kufanya hivyo, kupitia matendo yako utawaonyesha wanafunzi jukumu la msingi ambalo Roho Mtakatifu anatufanyia katika ugunduzi wa ufunuo katika kujifunza kwetu Neno.
3 Ukurasa 15 Ibada
4 Ukurasa 16
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
Made with FlippingBook - Share PDF online