Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 2 1 9
THEOLOJIA YA KANISA
Ili kupata maana ya Maandiko, wanafunzi wetu lazima wakubali jukumu lao kama wasomi na wanatheolojia. Kwa maana halisi, kila mtu mwenye maoni ya kitheolojia kuhusu jambo fulani la kidini ni mwanatheolojia. Jukumu la kujifunza ni kumtia moyo kila mwanafunzi kuwa mwanatheolojia wa kibiblia , anayepata ufahamu wake wa maisha kwa kujifunza kwa kina na kujishughulisha na Maandiko Matakatifu. Mifano hii ya kujenga darala kati yako na wanafunzi inalenga baadhi ya aina za maswali na masuala ya kawaida ambayo wanafunzi na wafanya wanafunzi wa Yesu watakutana nayo wanapojihusisha na wengine katika masuala yanayohusiana na Neno la Mungu, na kazi ya Bwana ulimwenguni. Tumia mifano hii kutambulisha mada kuu za masomo kwa njia ya kuangazia na kuleta uwazi juu ya masuala ambayo utakuwa unashughulika nayo unapoendelea na somo. Waambie wanafunzi washirikishane kwa ufupi (katika vikundi au darasa zima) kile walichochora na kwa nini. Kisha waulize wanafunzi, “Je, utambulisho wako kama mshirika wa Kanisa la Yesu Kristo ni sehemu tu ya yale yanayofahamika kama utambulisho wako, ama ushiriki wako katika Kanisa ndio ukweli muhimu unaokubainisha wewe ni nani?” Sisi kama The Urban Ministry Institute , tunatambua kwamba kuingizwa katika Kanisa kunapita na kubadilisha kila aina nyingine ya utambulisho wa kibinadamu. Kwa maana fulani, utambulisho wako kama mshirika wa Kanisa ni zaidi kama karatasi uliyochora kuliko alama/ishara zozote ulizozichora. Ni muktadha ambao katika huo utambulisho mwingine wowote hupata maana yake. Katika somo la leo tutajikita katika uelewa muhimu wa Kanisa kwa kusudi la kupata ufahamu wa kina kuhusu wokovu na maisha ya Kikristo. Wazo kuu la kitheolojia katika Maandiko yote ni kwamba vitu vyote vipo kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Neno kuu la Kiebrania ni kabod , wakati neno la Kiyunani doxa linatokana na dokeo , “kufikiri” au “kuonekana.” Neno kabod linatokana na kabed “kuwa mzito”, na linahusishwa na dhana za yule mwenye utukufu akiwa amejaa utajiri (Mwa. 31:1), mamlaka (Isa. 8:7), cheo au fahari (Mwa. 45:13), n.k. Ingawa wale waliotafsiri Septuagint walitumia doxa kutafsiri kabod , ni wazi kwamba kabod lilikuwa na wazo kubwa lililobeba maana zote mbili za heshima na sifa . Neno kabod linahusishwa na wazo la Mungu kujifunua kupitia madhihirisho ya nuru
5 Ukurasa 16 Kujenga Daraja
6 Ukurasa 17 Kujenga Daraja – Sehemu ya 2
7 Ukurasa 18 Kipengele namba I
Made with FlippingBook - Share PDF online