Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

2 2 0 /

THEOLOJIA YA KANISA

au kupitia kuonekana kwa Mungu katika sura za kibinadamu katika vipindi vya Agano la Kale, vinavyojulikana kama “theofania.” Dhana ya Mungu kama Mmiliki wa utukufu wa kimungu, na kama Yeye anayestahili sifa na heshima zote kwa sababu ya ukamilifu wake usio na mwisho ni wazo kuu linalojirudia katika ufunuo wote wa Maandiko. Shauku ya Musa ya kushuhudia asili ya ajabu na uso wa ajabu wa Bwana inafupishwa katika ombi lake kwa Mungu “Nionyeshe utukufu wako” (Kut. 33:18). Utukufu kwa maana hii si kitu kingine isipokuwa nafsi ya Bwana, ni ufunuo wa msingi wa jinsi Mungu alivyo katika Yeye Mwenyewe. Lugha isiyo ya kawaida, lakini hayo ndiyo maajabu ya Mungu tunayemtumikia! Utukufu wa Mungu si kitu kinachoongezewa juu yake bali ni sehemu kuu na ya msingi ya Yeye alivyo ndani ya nafsi yake ya ndani kabisa, ukuu wake, fahari yake, “utukufu” wake. Utukufu huu unaweza kuambatana na ishara fulani ya nje au inayoonekana kama ilivyokuwa katika maono haya, lakini haupaswi kulinganishwa na kitu chochote kile ambacho wanadamu wanaweza kuona au kuelewa. Utukufu wa Mungu ulionyeshwa katika maono ya Isaya hekaluni (rej. Isa. 6:1-), na ulirejelewa katika Yohana 12:41, ambapo pia unahusiana na nafsi ya Yesu Kristo, jambo ambalo linaweka uhusiano wa karibu kati ya Yesu na utukufu wa Mungu (rej. Yoh. 1:14-18). Katika Agano Jipya, dhana ya utukufu inahusu ukuu wake kamili kama Muumba (Rum. 1:23) pamoja na ukamilifu wa Mungu, na kwa kuzingatia wanadamu, hasa haki ya utukufu wa Mungu ambayo sasa inaonyeshwa katika wokovu wake katika Yesu Kristo (Warumi 3:23). Utukufu wa Mungu unaonyeshwa kikamilifu na kwa upekee katika sura ya Yesu Kristo (2 Kor. 4:6; Ebr. 1:3; Yoh. 1:14-18), ambaye mwenyewe ni ufunuo kamili wa nafsi yenye utukufu ya Baba mwenyewe, ambayo haiwezi kushuhudiwa kwa jicho la mwanadamu (kumbuka kwamba Baba anatajwa na Paulo kama “Baba wa utukufu” katika Efe. 1:17). Utajiri wa utukufu wa Mungu, kama Mwenye utukufu na kwa sababu hiyo anayestahili kutukuzwa, unaonyeshwa katika rejea ya Paulo anapouzungumzia utukufu wa Mungu katika lugha ya “utajiri” (Efe. 1:18; 3:16) na nguvu na uweza (Kol. 1:11). Mungu anaonyesha ajabu ya uweza wake mkuu na fahari isiyo na kikomo katika ufufuo wa Yesu kutoka kwa wafu (Rum. 6:4 rej. Efe. 1:19-). Ni jambo lisilo na shaka yoyote kwamba Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ni mtukufu na anastahili heshima. Hili ndilo agizo la wazi la kiadili la viumbe vyote – kumpa heshima Yeye ambaye anastahili utukufu wote katika mambo yote (Ufu. 4:11).

Made with FlippingBook - Share PDF online