Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
/ 2 2 1
THEOLOJIA YA KANISA
Zingatia kimaalum tofauti hii na ukweli huu wakati wa majadiliano yako na wanafunzi, hasa uchaguzi wa kimiujiza wa Mataifa ili kujumuishwa katika ufalme wa Mungu na mpango wa wokovu. Huenda hili halitawagusa wanafunzi wako kwa nguvu inavyopaswa, lakini msisitizo wako hapa unaweza kuwekea mkazo nguvu ya ajabu ya uteuzi huu wa Mungu kupitia majadiliano mafupi nao juu ya uelewa na mtazamo wa waamini wa wakati ule kuhusu Mataifa. Mtu anapotazama dhana ya Mataifa katika Biblia, ni rahisi kuona kwa nini uteuzi wa Mungu wa Mataifa ni ufunuo wa ajabu wa fadhili na neema ya Mungu, na inaonekana kuwa hauendani kabisa na taswira ya kawaida kuhusu Mataifa inayoonekana katika Neno la Mungu. Wanajumuisha mataifa yote ambayo si Wayahudi (Rum. 2:9; 3:9; 9:24) na wanaitwa kwa majina kadha wa kadha katika Maandiko, yakiwemo (katika SRB37) “wamizimu” (k.m., Zab. 2:1; Gal. 3:8), “mataifa” (Zab. 9:20; 29:20; 22:8; Isa. 14:6; 52:1), na “Wasiotahiriwa” (Rum. 2:26). Watu wa mataifa mengine wanaitwa Wayunani (Rum. 1:16; 10:12), wageni (Isa. 14:1; 60:10). Njia ambayo watu wa mataifa mengine wameainishwa katika Maandiko ingeonekana kuashiria kwamba hawakuweza au wasingeweza kamwe kujumuishwa katika makusudi ya wokovu wa Mungu. Sio tu kwamba wanaadhibiwa na kuhukumiwa na Mungu (k.m., 2 Nya. 20:6; Zab. 47:8; 9:5; 94:10), lakini wanaonyeshwa kama wasiomjua Mungu (Rom. 1:21; 1 Thes. 4:5), wameshikwa na hali ya kukataa kuwa na Mungu wala kumjua (Rum. 2:14), na kuwa waabudu sanamu waliojaa ushirikina (Rum. 1:23, 25; 1 Kor. 12:2; Kum. 18:14). Watu wa mataifa mengine wana sifa ya kuwa waovu, waliopotoka, waliojawa na lawama, na makufuru (Rum. 1:28-32; Efe. 4:19; Neh. 5:9), ambao hawamjui wala hawampendi Mungu wa kweli lakini wanaonyesha aina ya uaminifu potovu kwa miungu yao ya uongo (Yer. 2:11). Kwa sababu ya tabia hii mbovu na mwelekeo wa kuabudu sanamu, watu wa mataifa mengine wanaonyeshwa kuwa na migogoro ya kudumu na migumu na watu wa Mungu (Esta 9:1, 5; Zab. 44:13-14; 123:3), na watu wa Mungu hawatakiwi kufuata njia zao wala kuoana nao (rej. Law. 18:3; Yer. 10:2; Kumb. 7:3). Katika kuchunguza picha hii ya wale ambao hata wamesawiriwa katika Maandiko kama mbwa (rej. Mt. 15:26), ni jambo la kushangaza na la utukufu kwamba dhamira ya asili iliyofichwa ya Bwana wa mbinguni ilikuwa ni kuwakusanya Wayahudi na mataifa katika jamii moja mpya ya wanadamu ambayo ingefanyika watu wake wa ufalme milele (Efe. 2:11-22)!
8 Ukurasa 20 Kipengele namba II-C
Made with FlippingBook - Share PDF online