Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

2 2 2 /

THEOLOJIA YA KANISA

Kwa mara nyingine tena, umuhimu wa kujumuishwa kwa mataifa ni ukweli mkuu unaoweka msingi wa mapokezi ya Yesu duniani kote kati ya mataifa. Ni wazi kutokana na usomaji wa Maandiko kwamba watu wa mataifa mengine walipaswa kutengwa mbali na faida za Israeli, katika suala la uchaguzi na agano, angalau kwa kutazama kupitia historia ya Waisraeli (Efe. 2:11-12). Watu wa Mataifa hawakuruhusiwa kuingia hekaluni ( ona Mdo. 21:28-29), bali walizuiliwa penye ua wa nje (Efe. 2:14; Ufu. 11:2). Kupitia ukombozi, hata hivyo, ambao Kristo aliutoa kwa kifo na ufufuo wake, Mataifa sasa wamechukuliwa kama urithi kwa Kristo (Zab. 2:8), ambaye, kulingana na ushuhuda wa kinabii, aliangaza kama nuru kwao kwa ajili ya wokovu wao (Isa. 42:6; Lk. 2:32). Uongofu wa watu wa Mataifa unarejelewa katika Maandiko katika Isaya 2:2 na 11:10, na tofauti kati ya Myahudi na Mmataifa imeondolewa kwa njia ya Yesu Kristo (rej. Kol. 3:11; Gal. 3:28). Ingawa Injili haikuhubiriwa kwao mpaka baada ya Wayahudi kusikia habari njema katika Kristo (Mt. 10:5; Lk. 24:47; Mdo. 13:46), Injili iliwajia, kama ilivyoandikwa katika Matendo 10:34-45 na Mdo 15:14. Paulo alijitambulisha katika jukumu lake katika mpango wa wokovu kama Mtume wa Mataifa katika Matendo 9:15 na Wagalatia 2:7-8. Mungu, kwa wakati wake na namna yake, aliamua kwamba hatawaacha watu wa mataifa mengine pembezoni mwa upendo na neema yake, bali atawajumuisha katika mpango wake wa wokovu. Utambuzi huu wa ushirikishwaji wa Mataifa katika mpango wa Mungu ni kiini cha ufahamu wetu kuhusu kuipeleka Injili ulimwenguni kote kwa ajili ya Kristo (Mdo. 1:8; Mt. 28:18-20). Maswali haya yameundwa ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaelewa malengo muhimu na ukweli uliowasilishwa katika sehemu ya kwanza ya video. Utalazimika kupangilia muda wako vizuri, hasa ikiwa wanafunzi wako wanavutiwa na dhana hizi, na wanataka kujadili maana zake kwa urefu. Ruhusu muda ufaao wa kuangazia mambo muhimu ya somo, na bado uwe na muda wa kutosha wa mapumziko kabla ya sehemu inayofuata ya video kuanza. Ni muhimu sana uwasaidie wanafunzi kuona tabia thabiti na ya kimapinduzi ya upendo wa Mungu katika agano lake na Ibrahimu, pamoja na ufunuo wa fumbo la kujumuishwa kwa mataifa katika watu wapya wa Mungu. Uzito wa mafundisho haya hauwezi kupimwa; athari zake zinagusa kila eneo la maisha yetu.

 9 Ukurasa 22 Kipengele III-B

 10 Ukurasa 24 Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

Made with FlippingBook - Share PDF online