Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
2 3 4 /
THEOLOJIA YA KANISA
Imekuwa ikisemwa kwamba sakramenti ni kama saini kwenye hundi. Hazilingani na pesa halisi katika benki au shauku ya mtu anayetia saini kukuona unapewa fedha, lakini zinafanya hayo yapate kuonekana. Saini yenyewe haitakuwa na thamani lakini hutumika kama ishara inayoonekana ya kile ambacho mtu anatoa na hivyo ni ya thamani sana. Vivyo hivyo, sakramenti haina thamani yenyewe bali ina thamani kubwa kama ishara inayoonekana ya ahadi ya Mungu. Kanisa Katoliki linatambua sakramenti saba: ubatizo, Meza ya Bwana, kipaimara, kitubio, maagizo matakatifu (kuwekwa wakfu), ndoa, na upako wa wagonjwa (kupakwa mafuta kwa wagonjwa mahututi) pamoja na matendo mengi madogo yaitwayo “sakramenti” (kama vile ishara ya msalaba) ambayo pia inaaminika kutoa neema.
10 Ukurasa 52 Kipengele namba II-B
11 Ukurasa 52 Kipengele namba II-B-2
Baadhi ya makundi ya Wapentekoste, Wamennonite, na machache ya Kibaptisti pia wanafanya desturi za kuosha miguu kama agizo la ziada (taz. Yn. 13:14) pamoja na ubatizo na Meza ya Bwana.
12 Ukurasa 52 Kipengele namba II-C-1
Mfano wa kawaida ungekuwa kwamba ubatizo katika Agano Jipya hauokoi mtu hata kidogo kama ambavyo kutahiriwa katika Agano la Kale hakukuweza kumwokoa mtu. Iliwezekana kutahiriwa kimwili na bado kuchagua kuishi kama Myahudi mwabudu sanamu na asiyeamini. Tohara ilikuwa ishara ya Agano la Kale na ubatizo ni ishara ya Agano jipya. Zote mbili zimekusudiwa kuonyesha kwamba mtu kwa hakika ni sehemu ya watu waliochaguliwa na Mungu lakini mtu hapaswi kufanya kosa la kudhani kwamba ubatizo humfanya mtu kuwa Mkristo moja kwa moja. Hii ni kweli vile vile pasipo kujalisha kwamba mtu anaona ubatizo kama sakramenti au kama agizo.
13 Ukurasa 54 Kipengele namba III-A-2
Kwa maana hii, kubatizwa si jambo la hiari kama ambavyo haikuwa hiari kwa Waebrania kukataa kula Pasaka na kuweka damu kwenye miimo ya milango. Kuasi amri ya Mungu ilikuwa ni kujitenga na watu wa Mungu waliokuwa wakiokolewa. Utii katika hadithi ya Kutoka ulionyesha kwamba mtu alimwamini Mungu na
14 Ukurasa 55 Kipengele namba III-C
Made with FlippingBook - Share PDF online